Pata taarifa kuu
DRCONGO-M23-UN

Umoja wa Mataifa wapata matumaini ya kumaliza mgogoro mashariki mwa DR Congo

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa maziwa makuu Mary Robinson amesema mkataba wa hivi maajuzi wa amani unaojumuisha nchi 11 za ukanda huo umeonyesha uwepo wa matumaini ya kufikia amani katika eneo hilo.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Mary Robinson ambae ni rais wa Jamhuri ya Ireland ameyasema hayo jana wakati wa ziara yake jijini Goma mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na kaongeza kuwa Suluhu la mgogoro wa eneo hilo itapatikana kutokana na mchango wa pande zote husika na mgogoro huo.

Katika mazungumzo yake na Gavava Julien Paluku Kahongya, Robinson alisema kuwa amesikia mengi, ambayo atafanyia kazi mapema ili kuondoa hali ya wasiwasi na ukosefu wa usalama huko mashariki mwa DRC.

Kwa Upande wake Gavana wa Mkoa wa Kivu ya Kaskazini Julien Paluku pamoja na kuridhika na ziara hiyo, amesema kuwa kuna matumaini ya kufikia amani ya kudumu katika eneo hilo la mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Kabla ya kuondoka Mkuuhuyo alisema ataomba msaada wa jumla kwa mashirika ya kiraia, mashirika ya wanawake, vijana na makundi ya kidini ya kanda hii kushawishi serikali zao kuhusu utekelezwaji wa mkataba wa Addis Ababa.

Katika hatua nyinge hii leo kiongozi huyo anatarajiwa kuwasili nchini Rwanda baada ya kumaliza ziara yake huko DRC ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika kanda hii.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.