Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI

Idara ya usalama Marekani yaamuliwa kujiandaa kuhusu silaha za kemikali Syria

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa Serikali yake itafikiri upya juu ya hatua za kuchua ikiwa itabainika kuwa silaha za kemikali zilitumiwa na utawala wa Rais wa Syria, Bashar Al Assad.

REUTERS/Larry Downing
Matangazo ya kibiashara

Obama amesema kuwa idara ya ulinzi na Mashirika mengine ya Usalama yameamriwa kufanya maandalizi kwa hatua yeyote itakayochukuliwa ikiwa itabainika silaha za kemikali zilitumika.

Obama alizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ripoti ya kiintelijensia ya Marekani kuwa majeshi ya Syria yamekuwa yakitumia silaha za kemikali japo Marekani ilishaonya kuhusu matumizi ya silaha hizo.

Rais Obama amesema kuwa hawezi kuchukua hatua yoyote mpaka apate ukweli na kujiridhisha juu ya taarifa hiyo na endapo utawala wa Bashar Al Assad utadhihirika basi Marekani itachukua hatua kulingana na mapendekezo yaliyotolewa na vyombo vya usalama.

Serikali ya Assad imekuwa ikishutumiwa kutumia silaha hizo katika maeneo ya Makazi ya Raia huku, Balozi wa Syria ndani ya Umoja wa Mataifa, Bashar Jafaari akikana shutuma hizo akisema kuwa Wapinzani nchini humo wamekuwa wakitumia silaha hizo hasa walipofanya shambulizi karibu na mji wa Idlib nchini humo.

Serikali ya Syria imeikatalia timu ya wachunguzi kutoka umoja wa Mataifa kuingia nchini Syria na kuchunguza ukweli juu ya matumizi ya Silaha za kemikali katika mgogoro wa nchi hiyo ambao kwa mujibu wa Takwimu za Umoja wa Mataifa, Zaidi ya watu elfu sabini wamepoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.