Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-UN-AU

Kiongozi wa mapinduzi ya waasi Djotodia achaguliwa kuwa raisi wa mpito

Baraza la mpito nchini Jamhuri ya Afrika ya kati limemchagua kiongozi wa waasi ambaye aliongoza mapinduzi ya serikali mwezi uliopita Michel Djotodia, kuwa raisi wa mpito.

Kiongozi wa waasi wa Seleka nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati Michel Djotodia achaguliwa kuwa raisi wa mpito nchini humo..
Kiongozi wa waasi wa Seleka nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati Michel Djotodia achaguliwa kuwa raisi wa mpito nchini humo.. REUTERS/Alain Amontchi
Matangazo ya kibiashara

Djotodia, ambaye alijinadi kuwa raisi wa nchi hiyo baada ya waasi wa seleka kuchukua udhibiti wa mji mkuu wa Bangui amesema atahakikisha zoezi la uchaguzi linafanyika ndani ya miezi kumi na nane ijayo huku awali akisema lingefanyika baada ya miaka 3 kupita.

Raisi aliyekuwa madarakani Francois Bozize alikimbilia nje ya nchi hiyo mara baada ya harakati za waasi kuzidi kuuteka mji.
 

Awali Kanali Omar Bourdas ambaye ni mmoja wa maofisa wa Muungano wa Seleka alisema wapo katika mchakato wa kuimarisha na kuunda jeshi upya ili kuwa na jeshi litakaloweza kukabiliana na adui baada ya Seleka kutwaa nchi.

Naye Kanali Bourdas alisema wao watakuwa tofauti na Utawala wa Rais Francois Bozize ulioshindwa kuyaleta pamoja makundi nchini humo na kuchangia kuwepo kwa uasi kila kukicha.

Hadi sasa watu mia tatu wamejiandikisha wakitaka kujumuishwa kwenye Jeshi la Taifa wakiwemo wanaume na wanawake na mchakato wa kusaka wale wanaofaa kujumuishwa umeshaanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.