Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-CHAD-BENIN

Kiongozi aliyeangushwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Bozize aituhumu Chad kuusaidia Muungano wa Seleka kumng'oa madarakani

Kiongozi aliyeondoloewa madarakani kwa mapinduzi na kulazimika kukimbilia uhamishoni nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize amewatuhumu jirani zao wa Chad kutokana na kuusaidia Muungano wa Seleka kumuondoa madarakani.

Kiongozi aliyeomdolewa madarakani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize akiwa Ikulu wakati wa utawala wake
Kiongozi aliyeomdolewa madarakani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize akiwa Ikulu wakati wa utawala wake REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Bozize amezungumza kwa mara ya kwanza tangu serikali yake iangushwe na Muungano wa Seleka kutokana na Kundi hilo kukerwa na hatua ya kupuuza matakwa yao ambayo pande hizo zilikubaliana kwenye mazungumzo ya Libreville nchini Gabon.

Kiongozi huyo anayeishi uhamishoni kwa sasa amesema walifanikiwa kulisambaratisha Kundi la Seleka tarehe 23 ya mwezi Machi lakini siku moja baadaye wakapata taarifa kundi hilo linapata msaada kutoka kwa nchi moja Barani Afrika.

Bozize anaweka bayana baada ya kufanya uchunguzi wao wakabaini nchi hiyo ni Chad ambayo wamekuwa na uhusiano nayo wa kindugu kwa muda mrefu lakini walishangazwa na hatua waliyoichukua.

Kiongozi huyo anayesaka hifadhi ya ukimbizi nchini Benin kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje Arifari Bako anaweka bayana kuwa Kikosi Maalum cha Kijeshi kutoka nchini Chad ndiyo kiliendesha operesheni iliyoanza asubuhi ya jumapili na kushambulia kambi ya wanajeshi wa Afrika Kusini.

Chad ambayo ilikuwa msaidizi mkubwa kwa Bozize na kufanikisha kuingia kwake madarakani imetajwa kama Taifa linalostahili kutoa maelezo ya kina ili kufahamu sababu ya mapinduzi hayo kwa mujibu wa Kiongozi huyo.

Kauli ya Bozize inaweza ikapata nguvu kutokana na ripoti ya Shirika la Kimataifa la Kushughulikia Migogoro ICG kueleza kumekuwa na ishara za uwepo wa uhusiano kati ya Muungano wa Seleka na Utawala wa Chad.

Bozize pia ameanza kukosa hadhi ya urais baada ya kukatiliwa kushiriki kwenye Mkutano wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati ECCAS ambao utaketi kujadili mgogoro unaoendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mkutano huo utafanyika nchini Chad katika Mji Mkuu wa N'Djamena ambapo Kiongozi wa Muungano wa Seleka aliyejitangaza Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Michel Djotodia na Waziri Mkuu Nicolas Tiangaye watahudhuria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.