Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Serikali Mpya ya Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangaza Baraza lake la Mawaziri likiwa na Mawaziri Tisa kutoka Muungano wa Seleka

Serikali mpya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangazwa kuchukua nafasi ya ile iliyokuwa inaongozwa na Rais Francois Bozize iliyokuja kuangushwa na Muungano wa Seleka ukiongozwa na Michel Djotodia.

Kiongozi wa Muungano wa Seleka ambaye amejitangaza Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Michel Djotodia akiwapungia wananchi
Kiongozi wa Muungano wa Seleka ambaye amejitangaza Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Michel Djotodia akiwapungia wananchi
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Nicolas Tiangaye ametangaza serikali hiyo mpya ikiwa na wafuasi wachache wa Kundi la Seleka kipindi hiki ambacho Utawala huo ukilaumiwa kutokana na kufanya mauaji ya watoto katika Mji Mkuu Bangui.

Tiangaye ametangaza majina thelathini na wanne ambao wanatengeneza Baraza la Mawaziri kati yao tisa ni wafusai wa Muungano wa Seleka uliofanikishwa kuangushwa kwa serikali ya Rais Bozize.

Majina ya Mawaziri hao wanaounda Baraza Jipya la mawaziri yametangazwa kupitia Radio ya Taifa ambapo imejumuisha mawaziri wanane kutoka Chama cha zamani cha Upinzani pamoja na mkaribu mmoja wa Rais aliyeangusha Bozize.

Baraza la Mawaziri limeshuhudia Rais Djotodia aliyejitangaza kuchukua nafasi hiyo ya juu alijipa jukumu la kuwa Waziri wa Ulinzi kitu ambacho kinatajwa kimekuja kutokana na kuhofia anaweza akaangushwa kama akimpa jukumu hilo mtu mwingine.

Muungano wa Seleka umechukua nafasi nyingine nyeti kwenye Baraza la Mawaziri zikiwa ni pamoja na Wizara ya Mafuta, Wizara ya Maji na Misitu na Wizara ya Mawasiliano huku nyadhifa nyingine zikienda kwa mawaziri wengine.

Baraza hilo Jipya la Mawaziri limetangazwa ikiwa ni juma moja baada ya Muungano wa Seleka kufanikiwa kuiangusha serikali ya Bozize iliyokaidi kutekeleza matakwa yao ambayo yaliafikiwa katika Mkutano wa Libreville nchini Gabon.

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati inayoongozwa na Rais Djotodia imekanusha pia kutekeleza mauaji kwa watoto katika Mji wa Bangui kama ambavyo ripoti zilizotolewa zinavyoanisha.

Naye Waziri Mkuu Tiangaye amesema uteuzi wa Baraza la Mawaziri umezingatia pakubwa makubaliano ambayo yalifikiwa kwenye mazungumzo ya amani baina ya Serikali iliyoangushwa na Muungano wa Seleka yaliyofanyika Libreville.

Hofu ya kiusalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imeendelea kutanda huku wengi wakihisi kunaweza kukawa na mgawanyiko wa kidini baada ya Djotodia ambaye ni Mwislam kushika madaraka hatua iliyowakasirisha Waumini wa Kikristo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.