Pata taarifa kuu
SOMALI-MAREKANI

Marekani yajipanga kuitambua Serikali ya Somalia, Obama atangaza mpango wa kudhibiti silaha

Serikali ya Marekani inatarajia baadaye hii leo inatarajia kuitambua kwa mara ya kwanza serikali ya Somaliakatika kipindi cha miongo miwili tangu nchi hizo mbili zikatishe uhusiano wao baada ya Helkopta ya Washington kushambuliwa huko Mogadishu.

REUTERS/Larry Downing
Matangazo ya kibiashara

Kuanza kwa uhusiano mpya baina ya mataifa hayo mawili inakuwa ni matokeo ya ziara ya Rais Hassan Sheikh Mohamud huko Washington na anatarajiwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton.
 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Johnnie Carson anasema kutambuliwa kwa serikali ya Somalia kunadhihirisha kuanza upya kwa uhusiano wa mataifa hayo na kusaidia suala la usalama na hali ya kisiasa.
 

Wakati huohuo Rais wa Marekani Barack Obama ametangaza mpango wake wa kudhibiti matumizi ya silaha nchini humo na akitaka wale wote ambao watakutwa na makosa ya kushambulia wenzao wafungiwe pamoja na kuangalia uhalali wa wamiliki wa silaha hizo.

Rais Obama amesema huu ni wakati wa Baraza la Seneti kuketi na kujiridhisha na sheria zilizopo katika kuzuia matumizi mabaya ya silaha ambayo yamekuwa yakichangia vifo huku tukio alilolirejea ni kuuawa kwa watoto wa shule ishririni.

Kiranja huyo wa Dunia amewaambia wanahabari wakati umefika kwa serikali ya Marekani kuchukua hatua madhubuti zitakazokuwa ni mwarobaini wa matumizi mabaya ya silaha lakini ameshaanza kukosolewa kwa mapendekezo yake.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.