Pata taarifa kuu
IRAN

Iran yahofiwa kutengeneza bomu la Atomiki ndani ya miezi kadhaa

Iran huenda ikamudu kutengeneza Bomu la Atomiki kutokana na Madini ya Uranium yanayorutubishwa nchini humo ndani ya miezi miwili mpaka minne, wataalamu wa Maswala ya nuklia wameeleza.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Waandishi wa Ripoti mpya juu ya mpango wa Nuklia wa Iran, wamesema kuwa Tehran imeimarisha juhudi zake za urutubishaji wa Madini ya Uranium.

Ripoti hiyo iliyotolewa na Taasisi ya Sayansi na usalama wa kimataifa, imetoa viwango vya Urutubishaji kutoka kwa shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki IAEA.

Ripoti hiyo imekuwa na maoni sawa na Serikali ya Marekani kuwa ikiwa iran itafanya maamuzi ya kutengeneza Bomu, itawachukua miezi kadhaa tu kutengeneza bomu la Nuklia.

Iran yenyewe imekuwa ikikataa kujihusisha na utengenezaji wa silaha za Nuklia na kusisitiza kuwa mpango wake ni kwa ajili ya matumizi ya nishati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.