Pata taarifa kuu
ISRAEL-IRAN-MAREKANI

Waziri mkuu wa Israel ataka Iran ichorewe mstari wa mwisho kuhakikisha inaachana na mpango wake wa Nyuklia

Waziri mkuu wa Israe, Benjamin Netanyahu amesisitiza kauli yake kuhusu nchi ya Iran na kudai kuwa ni lazima nchi hiyo ichorewe mstari wa mwisho ili kuhakikisha inaachana na mpango wake Nyuklia.

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akizungumza wakati akihutubia wajumbe wa Umoja wa Mataifa mjini New York
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akizungumza wakati akihutubia wajumbe wa Umoja wa Mataifa mjini New York Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu Netanyahu ameyasema hayo siku ya Alhamisi wakati akihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambapo amesema kuwa iwapo jumuiya ya kimataifa haitaiwekea makataa nchini ya Iran kuhusu mapngo wake wa Nyuklia basi kuna hatari ya nchi hiyo kutekeleza azma yake ya ugaidi.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa muda wa kuizuia Iran kuendelea na mpango wa kurutibisha Nyuklia ni sasa na sio muda mwingine wowote na kwamba ni lazima tuchore mstari wa mwisho kwa nchi hiyo kuhakikisha haitengenezi silaha za maangamizi.

Ameongeza kuwa kuiwekea makataa ya mwisho nchi ya Iran haimaanishi kuanzisha vita na nchi hiyo bali inalenga kuizuia nchi hiyo kuendelea kuzalisha nyuklia kwa matumizi ya kutengeneza silaha za maangamizi.

Msemaji wa ofisi ya waziri mkuu, Mark Regev amesema kuwa "Je tuache muda upite huku Iran ikiendelea kuwa tishio la usalama wa dunia? au tuchukue hatua sasa kudhibiti nchi hiyo kuendelea kuzalisha silaha za maangamizi" hii ni njia pekee ya kuifanya Iran kuachana na mpango wake, alisema Regev.

Kwenye hotuba yake waziri mkuu Netanyahu amesema nchi yake inaushahidi kuonyesha kuwa nchi ya Iran hivi sasa inatumia asilimia sabini ya Uranium yake kutengeneza silaha za maangamizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.