Pata taarifa kuu
IRAN

Iran kufungua mkutano wa jumuiya ya nchi zisizofungamana na upande wowote hii leo.

Iran hii leo inafungua rasmi mkutano wa jumuia ya nchi zisizofungamana na upande wowote, mkutano ambao unaelezwa kutawaliwa na mjadala kuhusu Mpango wa Nuklia wa Iran. 

topnews.in
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon ametumia kipindi cha kuelekea mkutano kuwaambia Viongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei na Rais Mahmoud Ahmadinejad kuwa wanapaswa kuchukua hatua madhubuti kumaliza hali ya msuguano uliopo kuhusu Mradi wake wa Nuklia.

Halikadhalika shirika la kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA limeweka wazi uundwaji wa kikosi kazi kwa ajili ya kuchunguza mpango wa Nuklia wa Iran na kuangalia utekelezaji wa maazimio ya Umoja wa mataifa ikiwemo azimio la kukoma kwa mpango wa kurutubisha madini ya Uranium.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.