Pata taarifa kuu
Ujerumani

Mawakala wa Iran watiwa mbaroni nchini Ujerumani

Ujerumani imewakamata watu wanne wanaoshukiwa kuwa wamekuwa wakiisafirishia Iran mitambo ya kuendeleza mpango wake wa Nuclear.

Matangazo ya kibiashara

Polisi wanasema washukiwa watatu wameelezwa kuwa na uraia wa Ujerumani na Iran huku mmoja akiwa raia wa Ujerumani, na wametambuliwa kama Rudolf M, Kianzad Ka, Gholamali Ka, na Hamid Kh.

Washukiwa hao wanatuhumiwa kuwa wamekuwa wakifanya biashara ya kusafirisha mitambo hiyo ya nuclear kwa kipindi cha miaka miwili kinyume na sheria ya kibiashara kati ya Ujerumani na Iran,na walikamatwa na maafisa 90 wa usalama katika mji wa Hamburg.

Mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani yanashuku kuwa Iran inatengeneza silaha za Nuclear ambazo wanasema ni hatari kwa usalama wa dunia.

Hata hivyo,Iran inapinga tuhma hizo na kusema mitambo yake ni ya kufanya utafiti wa maswala ya teknolojia.

Mataifa ya Magharibi yamefumbia sikio maelezo ya Iran na kushuku Tehran  inatengeneza bomu la kushambulia mataifa hayo.

Umoja wa Ulaya pamoja na Marekani zimetangaza vikwazo dhidi ya uongozi wa rais Mahmud Ahmadinejad.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.