Pata taarifa kuu
SYRIA-IRAN

Shirika la Amnesty International lazionya pande zinazopigana kwenye mji wa Aleppo nchini Syria kuacha kutumia silaha nzito dhidi ya raia

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu duniani la Amnesty International limeonya dhidi ya kuendelea kutumika kwa silaha nzito kwenye mji wa Aleppo kati ya wanajeshi wa Serikali na waasi wa jeshi huru la Syria.

Moja ya maeneo ambayo yameshambuliwa kwa mabomu mjini Damascus
Moja ya maeneo ambayo yameshambuliwa kwa mabomu mjini Damascus Reuters/Shaam News Network/Handout
Matangazo ya kibiashara

Picha mpya za satelite zimeonesha kuongezeka kwa matumizi makubwa ya silaha nzito kwenye mji wa Aleppo na kuendelea kuzusha hofu kuhusu hali ya usalama wa wananchi ambao wamenaswa kwenye mji huo.

Wanaharakati nchini humo wamedai kuwa wamegundua zaidi ya mashimo makubwa 600 yanayoonekana kwenye mji wa Aleppo yamesababishwa na kutumika kwa silaha nzito kwenye makazi.

Shirika la Amnesty International limesema kuwa pande zote mbili zinazopigana kwenye mji huo zinawajibika kutokana na kile kinachoshuhudiwa na matatizo ambayo wananchi wanakumbana nayo wakati mapigano hayo yakiendelea.

Hapo jana waangalizi wa Umoja wa Mataifa UN waliamua kuondoka kwenye mji huo kwasababu za kiusalama baada ya kuongezeka kwa mashambulizi ya anga yanayofanywa na majeshi ya Syria.

Juma hili ujumbe maalumu wa Iran umesafiri hadi mjini Damascus kukutana na rais Bashar al-Asad, ujumbe ulioongozwa na mpatanishi wake Saeed Jalili ambaye anakutana kwa mara ya pili na utawala wa Syria.

Ujumbe huo uko nchini Syria kujaribu kushawishi kundi ambalo linawashikilia raia wake zaidi ya 48 ambao liliwateka jumapili iliyopita wakiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege.

Waasi wa Syria wamekuwa wakiituhumu Serikali ya Iran kwa kuendelea kuiunga mkono serikali ya Asad ambayo wamedai ni haramu na katili kwa kuendelea kuwaua wananchi wasio na hatia.

Hii leo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Ali Akbar Salehi amesema miongoni mwa raia wake waliotekwa mmoja kati yao ni mwanajeshi mstaafu wa jeshi la nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.