Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-MAREKANI

Clinton: Afrika Kusini inamchango mkubwa katika maendeleo ya bara la Afrika

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton ameitaka nchi ya Afrika Kusini kuwa mstari wa mbele katika kuunganisha nchi nyingine barani humo kupigania demokrasia na kuimarisha uchumi wao.

Hillary Clinton waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani ambaye yuko ziarani nchini Afrika Kusini
Hillary Clinton waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani ambaye yuko ziarani nchini Afrika Kusini Reuters
Matangazo ya kibiashara

Clinton ameyasema hayo wakati wa mkutano wake na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Kwenye mazungumzo yao, waziri Clinton ameitaja nchi hiyo kama mfano bora wa kuigwa na mataifa mengine barani Afrika katika kusimamia rasilimali zake na kuhakikisha serikali inaboresha maisha ya wananchi wake.

Waziri huyo ameongeza kuwa nchi hiyo inamchango mkubwa kwa dunia na ndio maana mataifa mengi barani Ulaya na Amerika yamekuwa yakishirikiana na nchi hiyo katika kujadili matatizo mbalimbali yanayoikabili dunia.

Clinton pia amezungumzia mgogoro wa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mashariki mwa nchi hiyo pamoja uhusiano wake na nchi ya Rwanda ambayo inatajwa kuwafadhili waasi.

Baadae hii leo waziri Clinton anatarajiwa kukutana na mkuu mpya wa tume ya Umoja wa Afrika AU Nkosazan Dalmini-Zuma aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo badala ya Jean Ping aliyemaliza muda wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.