Pata taarifa kuu
SYRIA

Vikosi vya majeshi ya Syria kukabiliana na waasi ili kurejesha mji wa Allepo

Vikosi vya serikali nchini Syria vinajiandaa na mashambulizi makali kwenye mji wa Allepo huku upinzani nao ukiripotiwa kujiandaa kukabiliana na majeshi ya serikali hali inayoashiria hatari kwa wananchi wa mji huo.

Reuters/Sana/Handout
Matangazo ya kibiashara

Ripoti kutoka nchini humo zinasema kuwa wanajeshi wa serikali wameuzunguka mji wa Allepo na wanapanga kushambulia wakati wowote huku jumuiya ya kimataifa ikionyesha hofu yake kuhusu kutokea kwa mauaji ya halaiki yanayoweza kufanywa na pande zote mbili.

Victoria Nuland ni msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani na yeye amekuwa wa kwanza kuonesha hofu yake kuhusu kutokea kwa mauaji ya halaiki.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon ameendelea kutoa wito kwa serikali ya syria na wanajeshi waasi nchini humo kusitisha mapigano na kurejea kwenye mazungumzo.

Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda nchini Syria kufuatia kuongezeka kwa makabiliano kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa jeshi huru la syria hali inayofanya kuongezeka kwa wimbi la wakimbizi kwenye nchi jirani.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.