Pata taarifa kuu
GUINEA BISSAU

Chama kikuu Guinea-Bissau chakataa mpango wa kuunda serikali ya mpito.

Chama kikuu nchini Guinea-Bissau PAIGC kimekataa wito uliotolewa na jeshi la mapinduzi nchini humo wa kuunda serikali ya mpito,ambayo itaratibu na kusimamia zoezi la uchaguzi ikiwa ni siku chache baada ya mapinduzi ya kijeshi.

Raisi wa mpito huko Guinea Bisau, Raimundo Pereira
Raisi wa mpito huko Guinea Bisau, Raimundo Pereira Liliana Henriques / RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kiongozi wa chama cha PAIGC alikiri chama hicho kukataa mapendekezo yoyote ambayo yapo kinyume na katiba yanayolenga kutatua mgogoro huo.

Chama hicho kimetaka raisi wa mpito Raimundo Pereira na aliyekuwa waziri mkuu Carlos Gomes ambao walitekwa usiku wa mapinduzi siku ya alhamisi kuachiwa huru mara moja.

Tangu uhuru mwaka 1974 ,jeshi la Guinea-Bissau na serikali imekuwa kkatika kutoelewana ambapo hakuna raisi aliyefanikiwakumaliza ngwe yake ya uongozi kutokana na kufanyika kwa mapinduzi kwa maraisi 3 na mwingine aliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.