Pata taarifa kuu
Senegal-Umoja wa Mataifa

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navy Pillay azitaka Guinea Bisau na Mali kuiga mfano wa Senegal

Mkuu wa tume ya haki za binaadam ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay amezitaka nchi za Mali na Guinea Bissau kufuata mfano wa Senegal katika mchakato wa uchaguzi ambao ulifanyika kwa uhuru, uwazi na haki.

Mkuu wa tume ya hazi za binadamu kwenye baraza la Umoja wa Mataifa Navy Pillay
Mkuu wa tume ya hazi za binadamu kwenye baraza la Umoja wa Mataifa Navy Pillay REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Akipongeza hatua iliyofikiwa na Senegal, Pillay amesema Mali pia ina rekodi nzuri ya kuwa na chaguzi zenye kufuata demokrasia kwa kipindi cha miongo miwili na kueleza matumaini yake kuwa hali ya Mali itarejea kama awali.

Majeshi ya Mali yalifanya mapinduzi dhidi ya Rais wa Mali Amadou Toumani Toure juma moja kabla ya kufanyika kwa duru la kwanza la uchaguzi wa Urais lililopangwa kufanyika tarehe 29 mwezi ujao.

Pillay ametoa wito kwa wagombea wa uchaguzi na wafuasi wao kujiepusha na utoaji wa matamshi yenye uchochezi halikadhalika ametaka vikosi vya usalama kutimiza wajibu wao kwa kufuata sheria wakati wote wa mchakato.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.