Pata taarifa kuu
IRAN

Wananchi wa Iran wanapigakura kuchagua wabunge wapya katika uchaguzi wa kwanza tangu mwaka 2009

Wananchi wa Iran wanapigakura kuchagua wabunge wapya kwa mara ya kwanza tangu nchi hiyo ifanye uchaguzi wake wa Rais uliomrejesha madarakani Mahmoud Ahmadinejad na hiki kinatazamiwa kuwa kipimo cha imani ya uongozi wake kwa wananchi wa taifa hilo linaloongozwa kwa misingi ya Sharia za Kiislam.

Wananchi wa Iran wakishiriki zoezi la kupigakura kuchagua Wabunge wapya nchini humo
Wananchi wa Iran wakishiriki zoezi la kupigakura kuchagua Wabunge wapya nchini humo REUTERS/Morteza Nikoubazl
Matangazo ya kibiashara

Huu ni uchaguzi mwingine kufanyika nchini Iran baada ya kushuhudia nchi hiyo ikipitia kwenye machafuko wakati wa Uchaguzi wa raia mapema mwaka elfu mbili na tisa kitu kilichochangiwa na Upinzani kupinga kwa nguvu zao zote ushindi wa Rais Ahmadinejad.

Wananchi hao wanapigakura kuchagua wabunge mia mbili na tisini kwa ajili ya Bunge la nchi hiyo licha ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani pamoja na Makundi ya Waislam wenye Msimamo Mkali kususia uchaguzi huo kutokana na Kiongozi huyo kuendelea kuweka kuzuizini nyumbani kwake kwa mwaka mmoja sasa.

Kiongozi wa Kidini nchini humo Ayatollah Ali Khamenei amekuwa ni miongoni mwa watu wa kwanza kupigakura kwenye uchaguzi huo kuhu akiendelea kusistiza nchi hiyo haiweze kurudi nyuma licha ya kuwekewa vikwazo na Mataifa ya Magharibi.

Khamenei amesema Mataifa ya Magharibi yamekuwa mstari wa mbele kuingilia Utawala wa Iran na hata kuituhumu kuhusiana na masuala ya Haki za Binadamu lakini ameweka bayana wataendelea kusimamia sharia zinazoongoza nchi hiyo.

Uchaguzi huo unaendelea kwa utulivu na tayari Mkuu wa Polisi Ahmadi Moghaddam amesema kila sehemu wameimarisha usalama katika kuhakikisha kila mwananchi anapigakura kwa utulivu na kisha kurejea kuendelea na shughuli zake.

Mapema Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje nchini Iran Ramin Mehmanparast amesema ushiriki mkubwa wa wananchi katika uchaguzi huu wa Wabunge itakuwa ni kinga kubwa kwa mapinduzi ambayo yanapangwa na maadui wa serikali.

Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje amesema wananchi walishaamua iana ya uatawala ambao wanautaka na hivyo kushiriki kwao kwenye uchaguzi kutaonesha ulimwengu demokrasia ya ukweli iliyopo nchini Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.