Pata taarifa kuu
Iran-Nyuklia

Ujumbe wa IAEA umekiri kushindwa kufikia muafaka na serikali ya Iran

Ujumbe wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani IAEA umekiri kushindwa kufikia muafaka na serikali ya Iran kutokana na kuzuiliwa kufika katika baadhi ya maeneo kujionea hali ya uzalishaji wa nyuklia. Ujumbe huo uliomba kuzuru katika kituo cha Parchin kilicho karibu na Téhéran ambako kulifanyika majaribio siku za nyuma, lakini hawakuruhusiwa na viongozi wa serikali ya Teheran, hivyo kuamuwa kuondoka nchini humo bila hata hivyo kuwa na lolote kuhusu mpango wa Nyuklia wa Iran

Herman Nackaerts, kiongozi wa ujumbe wa IAEA nchini Iran
Herman Nackaerts, kiongozi wa ujumbe wa IAEA nchini Iran REUTERS/Herwig Prammer
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo umeondoka Tehran baada ya kukaa kwa siku mbili wakiwa na lengo la kuthibitisha kama kweli Iran inatengeneza silaha za nyuklia kama ambavyo imekuwa ikituhumiwa na mataifa ya magharibi.

Taarifa ambayo imetolewa na IAEA imeonesha kusikitishwa kwake kwa kushindwa kufikia muafaka wa kile ambacho kilikuwa kimekubaliwa baina ya pande hizo za kufanya uchunguzi wa utengenezwaji wa silaha hizo za nyuklia au la.

Katika siku kumi na tano zijazo utafanyika mkutano wa wajumbe wa IAEA jijini Vienna, mkutano ambao shirika la nguvu za atomiki Duniani unasisitiza kutaka kupata majibu katika maswali kadhaa kutoka kwa viongozi wa Iran.

Iran imeonekana kupinga kutowa majibu katika maswala kadhaa yanayoulizwa, jambo ambalo linatia hofu huenda nchi hiyo inatengeneza bomu la Atomiki.

Ujumbe huo ulikuwa umekwenda nchini Iran kufanya uchunguzi kuhusu uwezo wa Iran katika urutubishwaji wa madini ya Uranium, baada ya ripoti iliotangazwa sana kwenye vyombo vya habari ilioishutumu Iran kuendeleza urutubishwaji wa Uranim kwa kutaka kutengeza bomu za maangamizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.