Pata taarifa kuu
SOMALIA

AU yatoa wito wa usaidizi kwa UN katika kupambana na alshabab

Mataifa ya Afrika yametoa wito wa usaidizi wa kutoka jumuia ya kimataifa kwa ajili ya majeshi yanayopambana na waasi wa Kiislamu nchini Somalia.

Askari wa jeshi la AMISOM
Askari wa jeshi la AMISOM REUTERS/Stuart Price
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Afrika umelitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kuongeza idadi ya walinda amani nchini Somalia kutoka elfu kumi na mbili mpaka elfu kumu na saba mia saba thelathini na moja.

Halikadhalika umoja wa mataifa umesema msaada wa fedha unahitajika kwa ajili ya vikosi hivyo vinavyopambana na wanamgambo wa Al Shabaab.

Hivi sasa jeshi la AMISOM lina vikosi 9000 kutoka Burundi, Uganda na Djibouti, chini ya Mpango wa umoja wa Afrika, ambapo nchi hizo tatu zitaongeza wanajeshi zaidi huku vikosi vya Kenya vilivyo nchini Somalia kupambana na Al Shabaab vitaendeleza Operesheni hiyo chini ya AMISOM.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.