Pata taarifa kuu
GUINEA BISSAU

Raisi wa Guinea Bissau Malam Bacai Sanha afariki dunia

Kiongozi wa taifa linalokabiliwa na machafuko katika eneo la ukanda wa Afrika magharibi Guinea Bissau Malam Bacai Sanha amefariki dunia akiwa nchini ufaransa ambako alikuwa anapatiwa matibabu.

Aliyekuwa raisi wa Guinea Bissau Malam Bacai Sanha
Aliyekuwa raisi wa Guinea Bissau Malam Bacai Sanha RFI
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya serikali ya Ufaransa imethibitisha kutokea kwa kifo cha raisi Sanha ambaye alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kukabiliwa na maradhi kabla hata ya sikukuu ya christmass.

Licha ya kiongozi huyo kulazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu hakuna taarifa rasmi ambazo zilitolewa kueleza ugonjwa ambao ulikuwa unamkabili hadharani.

Rais Sanha ambaye serikali yake ilitaka kupinduliwa na wanajeshi walioasi wakati akiwa anapatiwa matibabu huko Paris amekuwa akiendelea nchi hiyo licha ya uwepo wa hatari ya kupinduliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.