Pata taarifa kuu
ISRAEL-MAREKANI-UINGEREZA-URUSI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN lalaani ujenzi wa makazi unaofanywa na Serikali ya Israel

Mataifa ya Ulaya wameongoza kundi la nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN kulaani hatua ya Israeli kuendeleza makazi yake kwenye eneo la mpaka na kuongeza mapambano baina yao na Mamlaka ya Palestina.

EUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Ureno ni miongoni mwa nchi ambazo zimeungana kupinga kwa nguvu zao zote hatua ya kuendelezwa kwa makazi ya kiyahudi ambayo yamekuwa kikwazo cha kumaliza mgogoro wa mashariki ya kati.

Mataifa hayo yamesema kuwa kuendelea kwa ujenzi wa makazi mapya ya wayahudi yanatishia juhudi za kupatikana kwa amani ya kudumu kwenye eneo la Mashariki ya Kati licha ya mazungumzo kufanyika bila muafaka mara kadhaa.

Nchi hizo nne mwanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN zimetaka hatua madhubuti zichukuliwe dhidi ya serikali ya Israel kutokana na kuendelea kukaidi amri ya kusitisha ujenzi huo.

Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa UN Mark Lyall Grant amesema wakati umefika sasa kwa Israeli kusitisha ujenzi huo ili kupata amani ya kudumu kwenye eneo la Mashariki ya Kati.

Balozi Grant amekiri iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa ni wazi kabisa mahusiano baina ya Israel na Palestina yataendelea kusuasua na wala mkataba wa amani hauwezi kufikiwa kamwe.

Kwa upande wake nchi ya Urusi imeendelea kushindwa kuweka msimamo madhubuti juu ya suala hilo kwani Balozi wake kwenye Umoja wa Mataifa UN Vitaly Churkin amegwaya kulaani ujenzi wa makazi unaofanywa na Israel kwenye eneo la Palestina.

Brazil nayo imesimama imara na kulaani kile ambacho kinafanywa na serikali ya Israel cha kuendelea na makazi hayo ambayo yametakiwa kusimama ili kuhakikisha mkataba wa amani unafikiwa.

Balozi wa Brazil katika Umoja wa Mataifa UN Maria Luiza Ribeiro Viotti amesema ujezni huo ni kikiwazo kikubwa cha kufikiwa kwa amani kwenye eneo la Mashariki ya Kati na iwapo hatua hazitachukuliwa hakuna kitakachofanikiwa.

Israel imekuwa ikifanya ujenzi wa makazi mapya kwenye eneo la mpaka wa Palestina ambalo nchi hiyo linadai kuwa ni halali yake huku wenzao wakipinga na kusema wamevamia eneo lao.
Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.