Pata taarifa kuu
AUSTRALIA

Shirika la ndege la Australia, Qantas laanza kurusha ndege zake baada ya kusitisha huduma hiyo siku ya Jumamosi

Shirika la ndege la Australia, Qantas hatimaye limeanza tena safari zake baada ya kusitisha kufanya safari toka siku ya jumamosi kutokana na uongozi wa shirika hilo kuwa na mgogoro na shirikisho la wafanyakazi.

Mkurugenzi wa shirika la Qantas, Alan Joyce
Mkurugenzi wa shirika la Qantas, Alan Joyce REUTERS/Daniel Munoz
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya shirika hilo kutangaza kuanza kazi zake hii leo imekuja kufuatia amri ya mahakama huru nchini humo kuutaka uongozi wa shirika hilo kuanzisha safari zake wakati mgogoro kati yake na shirikisho la wafanyakazi na serikali unashughulikiwa.

Jumamosi ya juma lililoisha mkurugenzi wa shirika hilo Alan Joyce alitangaza shirika hilo kusitisha huduma zake za anga kwa muda kutokana na mgogoro huo ambao alieleza kuwa ulikuwa unawasababishia hasara ya dola milioni 15 kwa wiki.

Joyce amesema kuwa tayari shirika lake limepokea barua toka kwa mamlaka ya anga nchini humo kuruhusu ndege zake kuanza safari upya kama ilivyokuwa kawaida ili kuwaondolea usumbufu wananchi waliokuwa wakitegemea shirika hilo.

Mgomo wa wafanyakazi wa shirika hilo ulikuja kufuatia uongozi kutangaza kuwa unampango wa kupunguza zaidi ya wafanyakazi 1,000 mpango ambao toka mwezi wa nane mwaka huu uongozi umekuwa ukivutana na shirikisho hilo la wafanyakazi.

Mapema hii leo ndege za Qantas zimeshuhudiwa zikianza shughuli zake kama kawaida huku wafanyakazi wakiahidi kurejea tena katika mgomo wao endapo suala lao lisiposhughulikiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.