Pata taarifa kuu
LIBYA-NATO

Majeshi ya NATO nchini Libya kuhitimisha operesheni zake rasmi hii leo

Operesheni ya Kijeshi ya Majeshi ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO nchini Libya inatarajiwa kumalizika rasmi usiku wa leo wakati huu ambapo taarifa zinaeleza kuwa Viongozi wapya wa Libya watakabiliwa na hali ngumu ya kurejesha hali bora ya kisiasa.

Mitaa ya mji wa Sirte inavyoonekana hivi sasa baada ya mashambulizi ya NATO na waasi wa NTC
Mitaa ya mji wa Sirte inavyoonekana hivi sasa baada ya mashambulizi ya NATO na waasi wa NTC REUTERS/Esam Al-Fetori
Matangazo ya kibiashara

Majeshi ya NATO ambayo yalisaidia pakubwa kuangushwa kwa Utawala wa Hayati kanali Muammar Gaddafi yanatamatisha kibarua chake baada ya kuwasaidia vilivyo wapiganaji wa Baraza la Taifa la Mpito NTC kuondoa serikali iliyokuwa madarakani.

Kukamilika kwa Operesheni hiyo kunarejesha jukumu la ulinzi kwa majeshi ya NTC ambayo kwa mujibu wa Mustafa Abdel Jalil anayaona bado hayana uwezo wa kushika jukumu hilo katika kipindi hiki.

Majeshi hayo yanaondoka wakati shirika moja la kimataifa linalosimamia haki za binadamu duniani likitoa taarifa mpya ikionyesha kuwa kuna makundi ya wapiganaji wanaodaiwa kuwa wafuasi wa kiongozi aliyeuawa Kanali Muamar Gaddafi wakifanya mashambulizi ya kulipiza kisasi katika mji wa Misrata.

Kumekuwa na maswali mengi kuhusu walipo baadhi ya wanajeshi waliokuwa wakiunda jeshi la nchi hiyo ambao mpaka sasa wengi wao hawajulikani walipo huku silaha nyingi zilizokuwa zikimilikiwa na jeshi la Gaddafi pia zikiwa hazijulikani zilipo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.