Pata taarifa kuu
LIBYA

Makamanda wa NTC huko Misrata wasema maiti ya Kanali Muammar Gaddafi haitofanyiwa uchunguzi

Makamanda wa Wapiganaji wa Baraza la Taifa la Mpito Nchini Libya NTC waliopo katika Jiji la Misrata wamesema hakuna uchunguzi utaoafanywa dhidi ya maiti na Kanali Muammar Gaddafi aliyeuwawa huko Sirte lakini kitakachofanyika ni kuchungaza namna kifo chake kilichotokea.

Matangazo ya kibiashara

Makamanda hao wanakwenda kinyume na taarifa za awali ambazo zilitolewa na Utawala wa NTC ambao walisema kabla ya kuzikwa kwa mwili wa kanali Gaddafi ni lazima utafanyia uchunguzi kwa kuangalia majeraha aliyoyapata kwenye shambulizi lililochangia kifo chake.

Msemaji wa Wapiganaji wa NTC huko Misrata Fathi Al Bashaagha amesema hakuna uchunguzi utaoafanywa dhidi ya maiti ya Kanali Gaddafi leo wala siku yoyote kwani hakuna ambaye atafungua mwili wake.

Al Bashaagha ameongeza kuwa Mkuu wa Wapiganaji wa Utawala huo mpya Abdelhakim Belhaj anatarajiwa kuzuru Misrata kwa ajili ya kuangalia mwili wa Kanali Gaddafi aliyetawala kwa kipindi cha karibu miaka arobaini na miwili.

Kwa upande wake Kiongozi wa NTC Mustafa Abdel Jalil ameahidi kufanyika kwa uchunguzi wa kina juu kifo cha Kanali Gaddai kilivyotokea baada ya taarifa kusema wapiganaji walimkamata akiwa hai na kisha baadaye ndiyo wakamuua.

Umoja wa Mataifa UN, Serikali za Mataifa ya Kigeni pamoja na Mashirika ya Kutetea Haki za Binadamu Duniani yanataka kupatiwa taarifa namna ambavyo aliuawa Kanali Gaddafi baada ya kukamatwa huko Sirte akiwa hai.

Hatua hiyo ya kushinikizwa kufanyika kwa uchunguzi ndiyo inatajwa kuchelesha kufanyika mazishi ya Kanali Gaddafi aliyeuawa siku ya alhamisi kwenye operesheni ya NTC katika Mji wa Sirte ambalo alizaliwa kiongozi huyo.

Kifo cha Kanali Gaddafi kilipokelewa kwa shangwe na Viongozi wa Mataifa ya Magahribi ambao waliongoza mashambulizi dhidi ya serikali ya Kiongozi huyo chini ya Mwamvuli wa Majeshi ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO.

Mazishi ya Kanali Gaddafi huenda yakafanyika hii leo lakini taarifa zinasema sehemu ambayo mwili wake utahifadhiwa itakuwa siri ili kuwafanya wafuasi wake kutopata nafasi ya kuzuru eneo hilo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Usalama wa Taifa nchini Libya chini ya Utawala wa Kanali Gaddafi Abdullah Al Senussi anaelezwa kuwa amejificha nchini Niger serikali ya taifa hilo imethibitisha hilo.

Al Senussi ni miongoni mwa wanaosakwa na Mahakama Ya Uhalifu wa Kivita ICC kutokana na kufanya vitendo vya uhalifu wa kivita wakati ambapo maandamano ya kuupinga utawala wa Kanali Gaddafi yanafanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.