Pata taarifa kuu
LIBYA

Baraza la Mpito la Waasi Nchini Libya NTC latangaza kuhamishia makao makuu yake Tripoli juma lijalo

Viongozi wa Baraza la Mpito la Waasi nchini Libya NTC wamesema watahamishia rasmi Makao makuu ya Utawala wao katika Mji Mkuu Tripoli juma lijalo baada ya vikosi vyao kufanikiwa kuuangusha Utawala wa Kanali Muammar Gaddafi.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa Baraza la Mpito la Waasi NTC kutaka kuhamia Tripoli unakuja kutokana na kufanikiwa kusonga mbele na kuchukua maeneo zaidi ambayo yalikuwa chini ya vikosi vitiifu kwa kanali Gaddafi.

Kauli ya kuhamishia makao makuu ta Baraza la Mpito la Waasi NTC imetolewa na Mwenyekiti wake Mustafa Abdel Jalil akisema huko ndiko kunastahili kuwekwa ofisi zao na kuonesha utawala wao umekamilika.

Baraza la Mpito la Waasi NTC hapo awali lilipanga kuhamia Tripoli tarehe 26 ya mwezi August lakini wakabadili mawazo kwa kile walichosema ni kutaka eneo lote liwe na usalama wa uhakika ndiyo wafanye hivyo.

Uongozi huo mpya nchini Libya ambao unaungwa mkono na Mataifa ya uingereza, Ufaransa na Marekani unataka kujipanga ili kuweza kufanikisha ahadi yao ya kufanya uchaguzi wa wabunge mnamo miezi minane ijayo kabla ya kushuhudiwa uchaguzi wa Rais miezi ishirini toka sasa.

Huko Tripoli kumeendelewa kushuhudiwa sherehe ambazo zinaendelea kwenye Viunga vya Green ambavyo kwa sasa Waasi wamevipa jina la Martyrs ambapo maelfu ya wananchi wamejitokeza kuukaribisha utawala mpya.

Hatua hiyo inakuja wakati wananchi wakiendelea kuwakaribisha waasi kwa mikono miwili kwenye miji mbalimbali nchini Libya huku wakisubiri ahadi ya kufanyika kwa uchaguzi miezi ishirini baadaye.

Maelfu ya wananchi hao wakiwemo wanawake na watoto wamepongeza hatua ya kuelekea kuangushwa kwa utawala wa Kanali Gaddafi na kutaka Waasi wahakikishe demokrasia inachukua mkondo wake.

Sherehe hizi zinakuja wakati Kanali Gaddafi hapo jana ametuma ujumbe mzito akisema majeshi yake yapo tayari kupigana vita isiyo na mwisho na kusema utawala wake bado haujaangushwa.

Nchi ya Tripoli imeshuhudia vita iliyodumu kwa miezi sita ambapo Waasi wakisaidiwa na Majeshi ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO wamefanikiwa kuyasambaratisha majeshi ya knali Gaddafi ambaye kwa sasa hajulikani alipo huku familia yake ikikimbilia nchini Algeria kuomba hifadhi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.