Pata taarifa kuu
Serbia

Goran Hadzic mshukiwa wa mauaji ya kivita nchi Serbia akamatwa

Mamlaka nchini Serbia zimefanikiwa kumkamata kiongozi wa zamani wa kijeshi wa Serbia Goran Hadzic ambaye aliongoza vita dhidi ya nchi hiyo kati ya mwaka 1991 na 1995 na kuua maelfu ya raia.

Goran Hadzic, aliekuwa akitafutwa na mahakama ya TPIY hatiae amekamatwa
Goran Hadzic, aliekuwa akitafutwa na mahakama ya TPIY hatiae amekamatwa REUTERS/Stringer/Files
Matangazo ya kibiashara

Akiongea kupitia njia ya televisheni rais wa serbia Boris Tadich, amesema kuwa kukamatwa kwa Hadzic ni ushindi kwa taifa hilo na mhakama ya umoja wa mataifa katika kuwaska na kuwakamata wahalifu wa kivita waliohusika na mauaji ya raia wasio na hatia.

Mahakama maalumu ya umoja wa mataifa inayosikiliza kesi za viongozi wa serbia ilitoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi huyo akikabiliwa na makosa ya uhalifu wa kivita, ukiukaji wa haki za bindamu, ubakaji na mauaji ya waserbia.

Goran Hadzich alikamatwa katika milima ya Frusca Gora kaskazini mwa nchi hiyo na anatarajiwa kukabidhiwa kwenye mahakama hiyo muda wowote kuanzia sasa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.