Pata taarifa kuu
MAREKANI -URUSI

Rais Erdogan alaani hatua ya Marekani kutaka kuwakamata walinzi wake

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amelaani hatua ya maafisa wa usalama kutangaza hati ya kukamatwa kwa walinzi wake.

Walinzi wa rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akiwasambulia waandamanaji nchini Marekani
Walinzi wa rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akiwasambulia waandamanaji nchini Marekani voa
Matangazo ya kibiashara

Marekani inataka kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa walinzi 12 wa rais Tayyip kwa madai ya kuwapiga na kuwanyanyasa waandamanaji mwezi uliopita jijini Washington DC.

Kiongozi huyo wa Uturuki, ametetea hatua ya walinzi wake na kusema walikuwa wanamlinda dhidi ya magaidi.

Wizara ya Mambo ya nje ya Uturuki imesema imemwalika Balozi wa Marekani nchini humo ili kuzugumzia na kutatua hatua ya taifa lake.

Washington DC imesisitiza kuwa walinzi wa Tayyip hawana haki ya kuwavamia kundi la waandamanaji wa Kikurdi na Armenia waliokutana nje ya ubalozi wa Uturuki wakiwa na mabango ya kumpinga rais Tayyip.

Rais Tayyip alionekana akiwa anashuhudia kupigwa kwa waandamanaji hao huku akiwa amezingirwa na walinzi wake.

Uturuki imesema itapambana kisiasa na kisheria kupinga agizo hilo la Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.