Pata taarifa kuu
SIASA-MAREKANI

Sanders awasihi wafuasi wake kumuunga mkono Bi.Hillary Clinton kuwa rais

Mkutano mkuu wa chama cha Democratic nchini Marekani unaingia siku ya pili hivi leo mjini Philadelphia.

Bernie Sanders aliyekuwa anawania nafasi ya chama cha Democratic nchini Marekani kuwania urais
Bernie Sanders aliyekuwa anawania nafasi ya chama cha Democratic nchini Marekani kuwania urais REUTERS/Brian Snyder
Matangazo ya kibiashara

Siku ya kwanza ilitawaliwa na hisia mbalimbali kati ya wafuasi wa Bi. Hillary Clinton na Bernier Sanders waliokuwa wanapambana kutafuta tiketi ya chama hicho.

Baadhi ya wazungumzaji walizomewa na wafuasi wa Sanders wakati walipomnadi Bi.Clinton, hasa baada ya kubainika kuwa uongozi wa juu wa chama hicho ulikuwa unampendelea wakati wa kampeni za kutafuta tiketi ya chama hicho.

Bernie Sanders akihotubia mkutano mkuu wa chama cha Democratic mwaka 2016
Bernie Sanders akihotubia mkutano mkuu wa chama cha Democratic mwaka 2016 abc news

Hata hivyo, Sanders alionekana kuwaunganisha wafuasi wa chama hicho na kuwaomba kumuunga mkono Bi.Clinton na kuhakikisha kuwa anakuwa rais wa Marekani ifikapo mwezi Novemba.

Kabla ya kuanza kuzungumza, Seneta huyo wa jimbo la Vermont alishangiliwa kwa muda wa dakika tatu akiwa jukwani.

“Hillary Clinton ni lazima awe rais ajaye wa Marekani,” alisema huku akishangiliwa na maelfu ya wajumbe hao.

Michelle Obama akihotubia mkutano mkuu wa chama cha Democratic
Michelle Obama akihotubia mkutano mkuu wa chama cha Democratic REUTERS/Jim Young

Mke wa rais Obama, Mitchel Obama naye alihotubia wajumbe hao na kukashifu matamshi ya mgombea wa upinzani Donald Trump na kuongeza kuwa Bi.Clinton ndio mwanasiasa pekee wa kuaminiwa kuiongoza Marekani.

“Mtu asiwadangaye kuwa taifa hili sio kuu, eti kwamba kuna mtu anataka kulifanya kuwa kuu tena,” alisema huku akishangiliwa.

Ukumbi wa mkutano mkuu wa Democratic
Ukumbi wa mkutano mkuu wa Democratic Wtop.com

Leo ni siku ya rais wa zamani Bill Clinton ambaye pia ni mume wa Hillary kuhotubia wajumbe hao.

Rais Barrack Obama na Makamu wake Joe Biden, na mgombea mwenza wa Bi.Clinton Tim Kaine, wanatarajiwa kuzungumza kesho.

Hillary Clinton naye anatarajiwa kuwa mazungumzaji wa mwisho siku ya Alhamisi na atakaribishwa jukwani na binti yake Chelsea Clinton.

Baada ya kuidhinishwa rasmi na wajumbe hao, safari ya kupambana na Trump kuwania urais mwezi Novemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.