Pata taarifa kuu

Obama akutana na John Kerry kuzunngumzia mzozo wa mashariki ya kati

Rais wa Marekani Barack Obama anakutana na waziri wake wa mambo ya nje John Kerry kutathimini kuhusu mazungumzo ya Israeli na Palestina yanayo simamiwa na Marekani na ambayo hayaonyeshi sura nzuri kwa sasa baada ya pande mbili katika mazungumzo kuendelea kutiliana ngumu.

Matangazo ya kibiashara

John Kerry atatakiwa kutowa maelezo katika baraza la Congress kuhusu hatua za kuchukua wakati huu mazungumzo hayo ya mashariki ya kati yakiendelea kusuasua.

Kerry ambaye amerejea jijini Washington mwishoni mwa juma alisema anahitaji kukutana na rais Obama kuzungumzia kuhusu mzozo wa mashariki ya kati wakati huu Israeli ikitishia kuiwekea vikwazo Palestina ambayo inaendelea kudai nafasi kwenye taasisi za Umoja wa Mataifa.

Juma lililopita, mazungumzo kati ya pande hizo mbili yalionekana kugonga mwaba baada ya rais wa Mamlaka ya wa Palestina Mahmoud Abbas kuendelea kuonyesha nia ya kuomba nafasi katika taasisi za kimataifa.

hatuwa ambayo iliopelekea israeli kutishia kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Palestina iwapo inaendelea na hatuwa hiyo, na hata mpango wa kuwaacha huru wafungwa wa kipalestina ukasitishwa.

Marekani inafanya kila jitihada kuhakikisha pande hizo mbili zinarejea kwenye meza ya mazungumzo na muafaka unapatikana.

Wachambuzi wa maswala ya siasa wanaonakuwa wanaonakuwa mgogoro wa Israeli na Palestina utachukuwa muda mrefu kutatuliwa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.