Pata taarifa kuu

Ubelgiji yaitaka DRC kuwasilisha malalamiko dhidi ya Rwanda

Ubelgiji inaitaka Serikali ya Kongo kuwasilisha malalamiko dhidi ya Rwanda kwa mahakama za kimataifa kwa uchokozi. Kulingana na Radio OKAPI, balozi wa Ubelgiji mjini Kinshasa, Roxane de Bilderling, ndiye ambaye alitangaza haya siku ya Ijumaa Aprili 19 huko Goma mbele ya waandishi wa habari.

Waandamanaji wanazituhumu nchi za Magharibi kwa kushindwa kuilaani Rwanda inayodaiwa kuwaunga mkono M23
Waandamanaji wanazituhumu nchi za Magharibi kwa kushindwa kuilaani Rwanda inayodaiwa kuwaunga mkono M23 REUTERS - ANGE KASONGO ADIHE
Matangazo ya kibiashara

Hii ni baada ya kutaja sheria ya kutoshikika kwa mipaka ya kila nchi kama inavyotambuliwa na vyombo vya kisheria vya kimataifa.

Mwanadiplomasia huyo wa Ubelgiji alithibitisha, wakati huo huo, kwamba nchi yake ilikuwa tayari imelaani uchokozi wa Rwanda dhidi ya DRC kuhusiana na mauaji ya kikatili na yale yanayofanywa dhidi ya watu walio chini ya ulinzi wa vyombo vya dola yaliyofanywa katika ardhi ya Kongo:

“Ningependa kukumbusha hapa kwamba tulilaani uwepo wa wanajeshi wa Rwanda katika ardhi ya Kongo, tuliiomba Rwanda waziwazi kuwaondoa na kulaai kuwaunga mkono waasi wa M23. Tuliomba waziwazi. Na pia hizi ni jumbe ambazo zilipitishwa (...), wakati wa ziara ya waziri wetu mjini Kigali."

Lakini, kulingana na balozi huyo, matamko rahisi ya kulaani hayatoshi.

"Njia mojawapo ya kuweka shinikizo ni kwa Kongo kuwasilisha malalamiko katika Mahakama ya Kimataifa kuhusu kutoheshimiwa kwa mipaka ya kimataifa. Kwa sababu tayari Kongo imeshafanya hivyo dhidi ya nchi nyingine mfano Uganda na kupata mafanikio na fidia kwa kosa lililofanywa.”

Kutokana na habari hii, ikiwa ni pamoja na ripoti za wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, ambazo zinathibitisha kuwepo kwa wanajeshi wa Rwanda katika ardhi ya Kongo, alihoji Roxane de Bilderling, "kuna sababu ya Kongo kuwasilisha malalamiko katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki.

Roxane de Bilderling pia alipendekeza suluhisho la kidiplomasia na kisiasa ili kutatua mzozo wa usalama kati ya pande zinazohusika katika mzozo wa DRC.

Alikuwa sehemu ya ujumbe thabiti wa wanadiplomasia na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kibinadamu, kitaifa na kimataifa, wakiongozwa na Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu, Bruno Lemarquis. Ujumbe huo ulijumuisha kutathmini hali ya kibinadamu mashariki mwa DRC, kulingana na Radio OKAPI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.