Pata taarifa kuu

Zambia: Watu milioni waathiriwa na ukame

Takriban watu milioni 10 nchini Zambia wameathiriwa na ukame unaosababishwa na mfumo wa hali ya hewa ya El Nino, Makamu wa Rais Mutale Nalumango alisema siku ya Ijumaa.

WFP ikiwapa chakula wakaazi wa Simumbwe, Zambia (picha ya kielelezo).
WFP ikiwapa chakula wakaazi wa Simumbwe, Zambia (picha ya kielelezo). AFP - GUILLEM SARTORIO
Matangazo ya kibiashara

"Ukame umeathiri sana sekta ya kilimo, na kuharibu mazao ya msimu huu, na kusababisha tishio kwa usalama wa chakula nchini," Nalumango alisema kufuatia hadhara na Msaidizi wa Makamu wa Rais wa Idara ya Huduma za Jumla ya Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Guoqi Wu.

Akisisitiza kuwa wakulima wameathirika pakubwa kutokana na utegemezi wao mkubwa wa mvua, alibainisha kuwa serikali inawategemea washirika wake wa kimataifa kuunga mkono juhudi zake katika kutoa msaada wa chakula.

Kwa upande wake, Bw. Wu alielezea utayari wa IFAD kutoa msaada kwa serikali ya Zambia ili kukabiliana na athari za ukame, akikumbusha kuwa uhusiano na nchi hii ya kusini mwa Afrika umeimarishwa sana katika miongo ya hivi karibuni.

Mwezi Februari mwaka jana, Rais wa Zambia Hakainde Hichilema alitangaza kipindi cha ukame kuwa janga la kitaifa na dharura nchini humo.

Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni wiki hii, alisisitiza kuwa Zambia inahitaji zaidi ya dola milioni 900 ili kukabiliana na athari za ukame wa muda mrefu ambao umeikumba nchi hiyo tangu mwaka jana.

Nchi kadhaa kusini mwa Afrika zimekuwa zikikabiliwa na ukame mkali kwa miezi kadhaa unaosababishwa na mfumo wa hali ya hewa ya El Nino, na kuhatarisha mavuno ya nafaka kwa msimu wa sasa wa kilimo.

Kulingana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), athari za El Nino zilianza mwezi Oktoba 2023, zikiathiri hali ya hewa katikati ya hali ya hewa ya joto na mvua ya chini ya wastani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.