Pata taarifa kuu

RSF yaalaani kufukuzwa 'kiholela' kwa mwandishi wa habari wa Ufaransa nchini Togo

Shirika la Wanahabari Wasio na Mipaka (RSF) wameshutumu siku ya Jumatano kufukuzwa kwa "kinyama na kiholela" mwandishi wa habari wa Ufaransa kutoka Togo, anayejulikana kwa ukosoaji wake kwa serikali, wakati akitengeneza habari kuhusu mvutano wa kisiasa unaohusishwa na kupitishwa kwa Katiba mpya.

Mwezi Machi mwaka jana, waandishi wawili wa habari wa Togo walihukumiwa bila kuwepo mahakamani kifungo cha miaka mitatu jela kwa "kudharau mamlaka" na "kueneza uongo kwenye mitandao ya kijamii".
Mwezi Machi mwaka jana, waandishi wawili wa habari wa Togo walihukumiwa bila kuwepo mahakamani kifungo cha miaka mitatu jela kwa "kudharau mamlaka" na "kueneza uongo kwenye mitandao ya kijamii". © Reuters / Noel Kokou Tadegnon
Matangazo ya kibiashara

RSF inalaani vikali unyanyasaji wa kikatili na wa kiholela aliofanyiwa mwandishi Thomas Dietrich, ambaye anafanyia kazi jarida la mtandaoni la Afrique XXI, shirika hilo limesema katika taarifa yake.

Muda mfupi baada ya kuwasili Lomé siku ya Jumamosi, mwanahabari huyo anayejulikana kwa misimamo yake mikali kwa mamlaka ya nchi hiyo, alichapisha video kwenye X ambapo alielezea utawala wa Rais wa Togo Faure Gnassingbé kama "udikteta", ambao ungeimarisha madaraka yake kwa kupitishwa kwa Katiba mpya.

Rasimu hii itaifanya Togo kutoka utawala wa rais hadi utawala wa bunge; rasimu inayokataliwa na upinzani ambao unaona kuwa ni njia ya Faure Gnassingbé kusalia kama mkuu wa nchi kwa muda mrefu iwezekanavyo. Thomas Dietrich "alikamatwa na kutendewa ukatili na maafisa wa polisi kabla ya siku iliyofuata kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela kilichosimamishwa na kufukuzwa (siku ya Jumanne) kwenye ardhi ya Togo", inashutumu RSF.

Mwandishi huyo wa habari ameliambia shirika la habari la AFP kwamba "alipigwa, kuvuliwa nguo na kutukanwa" na maafisa wa polisi, baada ya mahojiano na mkuu wa Mamlaka ya uchunguzi wa vyombo vya habari na mawasiliano (HAAC).

Baada ya kukaa kizuizini kwa saa 24, alisema alihukumiwa na mahakama ya Lomé na kuhukumiwa kifungo cha miezi 6 jela, miaka 5 ya marufuku ya kuingia nchini Togo, na faini ya FCFA 600,000 (sawa na euro 916), kabla ya kufukuzwa na kuelekea Benin kwa kutumia gari.

Thomas Dietrich tayari amefukuzwa kutoka nchi ya nyingine ya Afrika. Mnamo mwezi wa Januari, alilazimika kuondoka Guinea wakati akichunguza Kampuni ya Kitaifa ya Mafuta (SONAP).

RSF pia inalaani kusimamishwa kwa muda kwa vibali vyote kwa vyombo vya habari vya kigeni vilivyotangazwa na HAAC siku ya Jumatatu, siku chache kabla ya uchaguzi wa wabunge na wa magavana uliopangwa kufanyika Aprili 29. HAAC inahalalisha uamuzi huu kwa "matatizo yanayohusishwa na mjumbe maalum Thomas Dietrich (...) katika muktadha wa kutoa vibali", na "mapungufu makubwa yaliyobainishwa katika uandishi wa habari za kisiasa nchini Togo na RFI na France 24 hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.