Pata taarifa kuu
USALAMA-SIASA

Libya yashindwa kupata suluhu baada ya kujiuzulu kwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa

Kujiuzulu kwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya, Abdoulaye Bathily, kunaashiria kushindwa kwa juhudi za maridhiano kati ya viongozi hasimu ambao aliwashutumu waziwazi kwa kuendeleza mgawanyiko wa nchi kwa ajili ya huduma kwa maslahi yao binafsi.

[Picha ya kielelezo] Abdoulaye Bathily, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Libya na mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL), katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tripoli mnamo Machi 11, 2023.
[Picha ya kielelezo] Abdoulaye Bathily, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Libya na mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL), katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tripoli mnamo Machi 11, 2023. AFP - MAHMUD TURKIA
Matangazo ya kibiashara

 

Akishikilia wadhifa huo kwa muda wa miezi 18 pekee, mwanadiplomasia wa Senegal, mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (Manul) alitangaza siku ya Jumanne kwamba amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, akinyooshea kidole cha lawama wahusika wakuu katika nchi iliyoathiriwa na machafuko na ghasia tangu kuanguka kwa utawala wa Gaddafi katikati ya majira ya kuchipua kwa nchi za Kiarabu mwaka 2011. Akibainisha "kuzorota" kwa hali katika miezi ya hivi karibuni, Bwana Bathily alishutumu "ukosefu wa nia ya kisiasa na nia njema ya viongozi wa Libya ambao wanafurahishwa na msukosuko wa sasa."

Nchi inatawaliwa naserikli mbili hasimu. Moja katika Tripoli (Magharibi) inaongozwa na Abdelhamid Dbeibah na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa, nyingine katika Mashariki, ni taasi na Bunge na lenye uhusiano na kambi ya Marshal Khalifa Haftar, ambaye ngome yake ni katika Benghazi. Uchaguzi wa urais na ubunge ulipangwa kufanyika mwezi Desemba 2021 lakini uliahirishwa kwa muda usiojulikana kutokana na tofauti kati ya kambi pinzani, na hivyo kurefusha hali ya sintofahamu ya kisiasa.

"Azimio la ubinafsi la viongozi wa sasa kudumisha hali iliyopo kwa ujanja na mbinu za kuchelewesha, kwa gharama ya watu wa Libya, lazima ikome," alisema Bw Bathily, ambaye pia alinyoosha kidole bila kutaja wafadhili wa kigeni wa wapinzani wa kambi zote mbili. . Kwa mujibu wa Jalel Harchaoui, mtafiti mshiriki katika Taasisi ya Royal United Services (RUSI), kuondoka kwa Bathily haishangazi "kwa sababu rahisi kwamba mchakato aliokuwa akiongoza kwa miezi kadhaa tayari ulikuwa umeshindwa kabisa."

"Hujuma"

Kwa mujibu wake, juhudi za Bwana Bathily kwa kiasi kikubwa zimedhoofishwa na Misri ambayo, pamoja na Falme za Kiarabu, ndiyo tegemeo kuu la kambi ya Marshal Haftar dhidi ya mamlaka ya Magharibi, inayoungwa mkono hasa na Uturuki.

"Hali hii ni matokeo ya mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na hasa sera ya Misri inayopingana kwa utaratibu na mantiki thabiti ambayo Bathily alijaribu kuingiza," mtaalamu huyu wa Libya ameliiambia shirika la habari la AFP. "Kutokana na hujuma ya Cairo, nchi za Magharibi zinzotetea demokrasia kama Marekani au Ufaransa hazijawahi, kwa njia ya kweli, kumuunga mkono Bathily, zikipendelea, kwa njia ya utulivu, kuepuka kuiudhi Misri," ameongeza.

Kwa Emad Badi, mtaalam katika Atlantic Council, kuondoka kwa Bathily kunakuja katika "hatua isiyoweza kupingwa ambapo hali ya utulivu iliyokuwepo nchini Libya katika miaka ya hivi karibuni inatoweka."

Huku tkukisubiriwa mrithi wake, ni Mmarekani Stephanie Koury, aliyeteuliwa mwezi Machi kama naibu wa Bw. Bathily kwa masuala ya kisiasa, ambaye atachukua nafasi ya muda. Williams alifanikiwa kuwaleta pamoja wawakilishi wa Libya mnamo Februari 2021 huko Geneva na kufikia makubaliano ya kisiasa na kuteuliwa kwa serikali ya mpito kuandaa uchaguzi wa rais na bunge mwishoni mwa mwaka 2021.

"Kuna uwezekano mkubwa" kumuona Bi Koury "akiibuka kama mjumbe maalum wa muda", ambao utakuwa "mpango unaoruhusu Marekani kuongoza UNSMIL bila kukabiliwa na kura ya turufu ya Urusi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa", anabaini Bw. Harchaoui. Jukumu lake la sasa kama naibu litamruhusu Bi. Koury kufanya kazi kama ya muda bila ya mkuu wa ujumbe, lakini bila kuungwa mkono na Baraza la Usalama, atakuwa "mipaka katika kile anachoweza kutimiza", amebaini kwa upande wake Badi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.