Pata taarifa kuu

Dolla za Marekani Milioni 160 zatolewa kuisaidia Ethiopia: UN

Umoja wa Mataifa unasema wahisani wa Kimataifa, wameahidi kutoa Dolla za Marekani Milioni 160, kushughulikia hali mbaya ya kibinadamu nchini Ethiopia, ambako watu Milioni 21 wanahitaji msaada hasa chakula.

Raia wa Ethiopia anakusanya sehemu za ngano ili kugawiwa kila familia inayosubiri baada ya kusambazwa na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama wa Tigray katika mji wa Agula, katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia mnamo Mei 8, 2021.  (Picha ya AP/Ben Curtis, Faili)
Raia wa Ethiopia anakusanya sehemu za ngano ili kugawiwa kila familia inayosubiri baada ya kusambazwa na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama wa Tigray katika mji wa Agula, katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia mnamo Mei 8, 2021. (Picha ya AP/Ben Curtis, Faili) AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Hii inakuja baada ya siku ya Jumane, wadau wa Kimataifa kukutana jijini Geneva kuchangisha Dola Bilioni 1 ambazo Umoja wa Mataifa unasema zinahitajika haraka kuwasaidia raia wa Ethiopia hasa walio kwenye jimbo la Tigray kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo.

Marekani imeahidi kutoa Dola Milioni 154, huku Umoja wa Ulaya ukiahidi kutoa Euro Milioni 131, wakati huu Umoja wa Mataifa ukisema unahitaji kwa haraka Dola Bilioni 1 kufanikisha kutoa misaada hiyo hadi mwezi Juni.

Mtoto akipita karibu na duka la muda lililofungwa katika kambi mpya ya wakimbizi ya Awulala, karibu na Maganan, kilomita 80 kutoka mpaka wa Sudan katika eneo la Amhara nchini Ethiopia, Februari 28, 2024. (Picha na Michele Spatari / AFP)
Mtoto akipita karibu na duka la muda lililofungwa katika kambi mpya ya wakimbizi ya Awulala, karibu na Maganan, kilomita 80 kutoka mpaka wa Sudan katika eneo la Amhara nchini Ethiopia, Februari 28, 2024. (Picha na Michele Spatari / AFP) AFP - MICHELE SPATARI

Raia wa Ethiopia wapatao Milioni 4, waliokimbia makaazi yao kutokana na mizozo ya ndani ya nchi hiyo, wanahitaji chakula wakati huu wengi wakisumbuliwa na utapia.

Soma piaEthiopia: Zaidi ya watu 400 wamefariki kutokana na njaa Tigray

Aidha, hali imeendelea kuwa mbaya baada ya mwaka uliopita, shirika la kutoa misaada la Marekani USAID na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP kusitisha msaada wake baada kuwepo kwa ripoti za wizi wa misaada hiyo.

Hillary Ingati- RFI-Kiswahili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.