Pata taarifa kuu

Watu wanane wa familia moja wafariki katika ajali ya boti nchini Msumbiji

Takriban watu wanane wa familia moja wamekuja maji nchini Msumbiji baada ya boti la wavuvi waliokuwemo kuzama kwenye Mto Zambezi, huku watu wawili wakinusurika na wengine wawili hawajulikani walipo, kulingana na viongozi kutoka eneo hilosiku ya Jumanne.

Hii ni ajali ya pili mbaya ya boti katika muda wa siku kumi nchini Msumbiji. (picha ya kielelezo)
Hii ni ajali ya pili mbaya ya boti katika muda wa siku kumi nchini Msumbiji. (picha ya kielelezo) © TVM/AFP
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lililotokea Jumatatu katika jimbo la Sofala (katikati) linakuja wiki moja baada ya ajali ya boti iliyozama  umbali wa kilomita 1,000 zaidi kaskazini mwa ufuo wa Msumbiji, ajali ambayo ilisababisha vifo vya watu 98, wakiwemo watoto wengi.

Watu kumi na wawili wa familia moja waliingia kwenye boti la mbao lisilo na injini, Nobre dos Santos, mkuu wa wilaya ya Caia ambako Mto Zambezi unapita, ameliambia shirika la habari la AFP, na kuongeza kwamba familia hii ya wakulima ilitaka kwenda kwao "Watu wawili walinusurika na wengine wawili bado hawajapatikana,” amebaini na kuongeza kuwa shughuli ya kuwatafuta watu hao unaendelea.

Mnamo Aprili 7,boti la wavuvi lililokuwa na watu wapatao 130 lilipinduka, na kuua watu wasiopungua 98. Boti hilo lililojaa mizigo lilibeba familia nyingi zilizojawa na hofu ambazo zilikuwa zikijaribu kukimbia baada ya uvumi wa ugonjwa wa kipindupindu.

Msumbiji, mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, imerekodi rasmi takriban kesi 15,000 za kipindupindu tangu Oktoba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.