Pata taarifa kuu

Ethiopia: Amnesty International yataka uchunguzi kuhusiana na mauaji ya raia eneo la Amhara

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limelitaka Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, kuichunguza Ethiopia kufuatia ripoti za mauaji ya raia yaliyofanywa na Jeshi la Taifa la Ethiopia katika mji wa Merawi, jimbo la Amhara.

Picha ya Shirika la Habari la Ethiopia linalomilikiwa na serikali, Nov. 16, 2020. (Ethiopian News Agency via AP)
Picha ya Shirika la Habari la Ethiopia linalomilikiwa na serikali, Nov. 16, 2020. (Ethiopian News Agency via AP) AP
Matangazo ya kibiashara

Mwaka uliopita shirika la Umoja wa mataifa liliripoti zaidi ya matukio 48 ya mauaji huko Tigray tangu mwaka 2020 wakati ambapo mkurugenzi mkuu wa Amnesty International katika eneo la mashariki na kusini mwa Afrika, Tigere Chagutah, akisema mauaji ya halaiki Ethiopia yanazidi kuwa ya kawaida.

Wakaaji wa Amhara waliambia Amnesty International kuwa mauaji hayo yalifanyika mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu huku baadhi waathirika wakiwa na majeraha ya risasi.

Chagutah anasema serikali haijaweka juhudi za kutosha kuhakikisha familia za waliouawa zinapata haki na anataka mataifa wanachama wa AU kuingilia kati na kuamuru uchunguzi wa mauaji ya raia.

Wanajeshi wa serikali walikuwa wanapigana na wanachama wa kundi la kujihami la Fano kabla ya kudaiwa  kugeukia raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.