Pata taarifa kuu

Jeshi la Burkina lapokea ndege zisizo na rubani kutoka Uturuki kwa vita dhidi ya wanajihadi

Jeshi la Burkina Faso lilipokea siku ya Jumatatu ndege kumi na mbili za kivita zilizotolewa na Uturuki kwa ajili ya kupambana na makundi ya wanajihadi, kulingana na ofisi ya rais wa Burkina Faso.

Ndege isiyo na rubani ya Bayraktar TB2 iliyotengenezwa na Uturuki imepigwa picha tarehe 16 Desemba 2019 katika kambi ya kijeshi ya Gecitkale karibu na Famagusta katika eneo linalojiita Jamhuri ya Uturuki ya Kupro ya Kaskazini (TRNC).
Ndege isiyo na rubani ya Bayraktar TB2 iliyotengenezwa na Uturuki imepigwa picha tarehe 16 Desemba 2019 katika kambi ya kijeshi ya Gecitkale karibu na Famagusta katika eneo linalojiita Jamhuri ya Uturuki ya Kupro ya Kaskazini (TRNC). AFP - BIROL BEBEK
Matangazo ya kibiashara

Ndege hizi zisizo na rubani - Bayraktar TB2 na Bayraktar Akinci - zilikabidhiwa kwa jeshi na mkuu wa utawala wa kijeshi, Kapteni Ibrahim Traoré, wakati wa hafla iliyorekodiwa na kutangazwa na ikulu ya rais.

"Majaribio yote yalikuwa ya uhakika, kwa hiyo ni jambo la kujivunia kuthibitisha kwamba ndege hizi zinajiunga na kikosi cha wanamaji cha jeshi la Burkina faso," alibainisha Kapteni Traoré, mbele ya Waziri wa Ulinzi, Jenerali Kassoum Coulibaly.

"TB2" "imeonyesha uwezo wako yenyewe tangu kuanza kwa vita hivi," amesema Bw. Traoré, akiongeza kwamba "Akinci" "imevuka uwezo wa kiufundi uliopangwa na mtengenezaji." "Upanuzi wa kikosi cha majini kwa hiyo hufanya iwezekanavyo kuingilia kati kwa wakati unaofaa" na kufanya "ufuatiliaji wa kudumu", aliongeza.

"Tuna wingi wa mashine za aina hii kwa sasa ziko angani zikifznya kazi, zikitafuta kupata na kuharibu adui yeyote kutokana na michango ya watu," Jenerali Coulibaly alisema.

Mkuu wa utawala wa kijeshi wa Burkina Faso alimshukuru Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kwa ushirikiano huu "salama na wa dhati". Baada ya kulipa kisogo jeshi la Ufaransa mwaka jana, Burkina Faso imejisogeza karibu na washirika wapya, ikiwa ni pamoja na Uturuki na Urusi.

Tangu mwaka wa 2015, nchi hiyo imekuwa ikikabiliwa na ghasia za wanajihadi zinazohusishwa na makundi yenye mafungamano na Al-Qaeda na Islamic State, pamoja na ulipizaji kisasi unaohusishwa na vikosi vya jeshi na wasaidizi wao, ambao umesababisha vifo vya watu 20,000 na milioni mbili kuyahama makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.