Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-SIASA

Upinzani nchini Togo waitisha maandamano baada ya uchaguzi wa wabunge kuahirishwa

Vyama kadhaa vya upinzani vya Togo na mashirika ya kiraia vimeitisha maandamano ya siku tatu siku ya Alhamisi kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa wabunge na wa magavana, huku kukiwa na mvutano wa kisiasa unaoongezeka tangu kupitishwa kwa Katiba mpya mwezi Machi.

Mikusanyiko ya hadhara inayoandaliwa na upinzani ni nadra na mara nyingi imepigwa marufuku tangu Machi 2020, baada ya kugunduliwa kwa kesi ya kwanza ya UVIKO-19 nchini Togo.
Mikusanyiko ya hadhara inayoandaliwa na upinzani ni nadra na mara nyingi imepigwa marufuku tangu Machi 2020, baada ya kugunduliwa kwa kesi ya kwanza ya UVIKO-19 nchini Togo. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Vyama vinne vya upinzani (ADDI, ANC, FDR na PSR) na shirika la kiraia (FCTD) "vinatoa wito kwa watu kuungana nao kwa maandamano makubwa Aprili 11, 12 na 13", katika taarifa iliyotolewa kwa umma siku ya Alhamisi, na. "wanaomba wagombea kuendeleza kampeni nchi nzima".

Maandamano yamepigwa marufuku nchini Togo tangu mwaka 2022, baada ya shambulio kwenye soko kubwa la Lomé ambalo lilisababisha kifo cha askari mmoja. Wito huu wa kuandamana umekuja siku moja baada ya kutangazwa kuahirishwa kwa uchaguzi wa wabunge na wa magavana, ambao awali ulikuwa umepangwa kufanyika Aprili 20, ili, kwa mujibu wa mamlaka, kutoa muda kwa Bunge kuisoma kwa mara ya pili rasimu ya Katiba mpya ambayo iliidhinishwa Machi 25.

Baada ya sintofahamu iliyosababishwa na kupitishwa kwa Katiba hii mpya, ambayo inaihamisha Togo kutoka utawala wa rais hadi utawala wa bunge, Rais Faure Gnassingbé - madarakani tangu mwaka 2005 akimrithi baba yake ambaye tawala nchi hii kwa karibu miaka 38 - wiki iliyopita aliagiza wabunge kufanya tathmini ya rasimu ya katiba.

Thomas Kokou N'soukpoe, msemaji wa Dynamique Monseigneur Kpodzro (DMK, kundi la vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia) ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi kwamba "wanachama tisa wa DMK walikamatwa jana (Jumatano), walipokuwa wakihamasisha watu katika soko la Akodessêwa kuhusu hatua iliyo kinyume cha sheria ya marekebisho ya katiba." "Kwa sasa, hatujui wanatuhumiwa nini," ameongeza. Polisi hawakujibu maombi kutoka kwa AFP kuhusu kukamatwa kwa watu hawa.

"Dharau"

Kuahirishwa kwa uchaguzi huo, bila tarehe mpya kutangazwa, "ni ishara ya dharau kwa wagombea ambao wamejitayarisha na ambao wametumia gharama kubwa, ni haraka sana," Brigitte Adjamagbo-Johnson, mratibu wa DMK, kundi la vyama vya upinzani vya kisiasa na mashirika ya kiraia, ameliambia shirika la habari la AFP.

Upinzani unahofia kwamba Katiba mpya, ambayo inalipa Bunge mamlaka ya kumchagua moja kwa moja rais na mkuu wa serikali, itatoa nafasi ya kwa Rais Faure Gnassingbé kusalia madarakani kwa kipindi kirefu.

"Watogo wana hasira na wanataka muswada huu wa kikatiba uondolewe tu," Nathaniel Olympio, rais wa chama cha  PT, ameliambia shirika la habari la AFP, ambaye anabaini kwamba serikali "iko katika mchakato wa kuleta machafuko katika nchi". "Watogo wako macho wakati huu, mapinduzi haya ya kikatiba hayatafanikiwa," aliongeza.

Uchaguzi wa wabunge na magavana ulipaswa kufanywa mwezi wa Desemba, kisha ukapangwa Aprili 12 kabla ya kuahirishwa hadi Aprili 20. Upinzani, ambao ulisusia uchaguzi uliopita wa wabunge mnamo mwaka 2018, unapanga kushiriki kwa wingi katika kura hiyo mwaka huu.

Mvutano wa kisiasa nchini Togo  ni sehemu ya Afrika Magharibi iliyotikiswa na mapinduzi nchini Mali, Guinea, Burkina Faso na Niger, pia harakati za wanajihadi zinazofanywa kaskazini mwa Togo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.