Pata taarifa kuu

Mali: Kumi na nane wauawa Diankabou wakati wa operesheni ya kijeshi

Nchini Mali, takriban raia 18 waliuawa katika vijiji kadhaa katika wilaya ya Diankabou siku ya Jumamosi Machi 30. Jeshi kwa ushirikiano na wanamgambo wa kundi la Wagner kutoka Urusi pamoja na wawindaji wa jadi wa Dozo walifanya operesheni ya kijeshi katika wilaya ya Bandiagara, katikati mwa Mali, katika randabauti ya Koro. Mbali na raia waliouawa, mamia ya ng'ombe waliripotiwa kuibwa, jambo ambalo baadhi ya vyanzo vinapingana.

Nembo ya vikosi vya jeshi la Mali. (picha ya kielelezo)
Nembo ya vikosi vya jeshi la Mali. (picha ya kielelezo) AFP - AGNES COUDURIER
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia saa 9 asubuhi hadi mwisho wa alasiri, walitoka kijiji hadi kijiji, wakivuka wilaya ya Diankabou. Kulingana na wawakilishi wengi wa jamii, viongozi wa kijadi au wakazi wa kawaida wa eneo ilo lililohojiwa na RFI, askari wa Mali, wakiandamana na mamluki kutoka kundi la Wagner na wawindaji wa jadi wa dozo - wawindaji hutumiwa mara kwa mara na jeshi kama waelekezi - walikuwa wengi sana.

Walifaya msako wa nyumba kwa nyumba huko Tan-Coullé, Tan-Ali, Tan-Samba na Bamguel. Msako ulifanyika bila vurugu, lakini "karibu watu ishirini" - 18 hadi 21 kulingana na vyanzo - waliokutana nje ya vijiji hivi, wakiwemo watoto, waliuawa kwa kupigwa risasi. Vyanzo kadhaa pia vinaripoti watu waliotoweka.

Wengine “waliogopa na walitaka kujificha,” chaeleza chanzo kutoka Diankabou. Wengine “walipumzika chini ya mti,” kilibaini chanzo kingine. "Hawakuwa magaidi, walikuwa mahali pasipofaa kwa wakati usiofaa," chanzo cha usalama cha Mali kinasikitika, ambacho kinathibitisha kwamba watu 18, ambao ni raia, waliuawa. Wanaume wawili pia walikamatwa "kwa uthibitisho" baada ya silaha kupatikana katika nyumba yao.

Hatimaye, vyanzo vingi vya ndani vinashutumu jeshi, na wasaidizi wake wa Wagner na wawindaji wa dozo, kwa kuiba angalau ng'ombe 400, wa familia kadhaa za Tan-Coullé. "Sio wizi," kinasema chanzo cha usalama cha Mali, "lakini kuna mzozo juu ya umiliki wa wanyama hawa." Gavana wa eneo la Bandiagara aliarifiwa, kazi inafanywa "kutambua wamiliki halisi" wa mifugo.

Gavana wala jeshi la Mali hawakutaka kujibu baada ya kuombwa na RFI kutoa maoni yao kuhusiana na tukio hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.