Senegal: AU yampongeza rais mteule Bassirou Diomaye Faye
Nairobi – Umoja wa Afrika, umempongeza rais mteule wa Senegal Bassirou Diomaye Faye ambaye alikuwa mgombea wa upinzani kwa ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa urais.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Katika taarifa yake, Tume ya Umoja wa Afrika kupitia mwenyekiti wake Moussa Faki Mahamat imemtakia Faye mema katika nafasi yake mpaya.
Kwa mujibu wa matokeo ya awali, Faye aliibuka mshindi wa uchaguzi huo katika duru ya kwanza kwa kupata asilimia 54.3 dhidi ya mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na rais Macky Sall, waziri mkuu wa zamani Amadou Ba.
Communiqué du Président de la Commission de l’Union africaine @AUC_MoussaFaki sur l’élection de Monsieur Bassirou Diomaye Faye Président de la République du Sénégal.
— African Union (@_AfricanUnion) March 29, 2024
https://t.co/pyKFJMUCad pic.twitter.com/o6uDLWhHMP
Mahakama ya katiba nchini Senegal inatarajiwa kumtangaza rasimi Faye kuwa mshindi wa uchaguzi huo kabla ya wikendi hii.
Faye, 44, aliachiwa kutoka gerezani siku kumi kuelekea tarehe ya uchaguzi huo akiwa na kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko, ambaye naye alizuiwa kugombea katika uchaguzi huo kutokana na mashataka ambayo alisema yalichochewa kisiasa.