Pata taarifa kuu

DRC: Rais Salva Kiir amekutana na mwenzake Felix Tshisekedi jijini Kinshasa

Nairobi – Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, jana alikutana na kufanya mazungumzo na rais wa DRC Felix Tshisekedi jijini Kinshasa, kujadili hali ya usalama na kisiasa kwenye ukanda, hasa uhusiano kati ya Kinshasa na Kigali.

Rais Kiir pia amezuru nchi za Rwanda na Burundi.
Rais Kiir pia amezuru nchi za Rwanda na Burundi. © RDC Statehouse
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya rais Kiir, imekuja baada ya kutembelea Rwanda na Burundi wiki kadhaa zilizopita, na akiwa jijini Kinshasa ametoa wito kwa rais Tshisekedi kutekeleza mikataba ya amani ya Nairobi na Luanda ili kusaidia kueleta amani ya kudumu Mashariki mwa DRC pamoja na nchi jirani ya Rwanda.

Aidha, Kiir amesema ataendeleza harakati za kuhakikisha kuwa suluhu ya kudumu inapatikana kati ya Rwanda na DRC na utulivu unarejea eneo la Mashariki, linaloshuhudia mapigano kati ya waasi wa M 23 na wanajeshi wa serikali.

Hata hivyo, rais Tshisekedi katika kikao na Kiir ameendelea kumshtumu rais wa Rwanda Paul Kagame kuwa kikwazo cha kupata amani ya kudumu kwa serikali yake kuunga mkono utovu wa usalama unaoendelea Mashariki mwa DRC, madai ambayo Kagame amekuwa akikanusha.

Baada ya kuzuru Kinshasa, rais Kiir amesema anatarajiwa kuzuru Luanda kukutana na rais wa Angola Joao Lourenco, msuluhishi wa bara Afrika kuhusu mzozo kati ya DRC na Rwanda, wakati huu ripoti zikisema kuwa viongozi wa nchi hizo jirani wameonesha utayari wa kukutana kwa ajili ya mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.