Pata taarifa kuu

Senegal: Uchaguzi wa urais kufanyika kesho Jumapili ya wikendi hii

Nairobi – Wananchi wa Senegal kesho, watapiga kura kumchagua rais mpya, katika uchaguzi uliosubiriwa kufuatia misukosuko ya kisiasa, baada ya kuahirishwa kwake kutoka mwezi Februari.

Wachambuzi wa siasa za Senegal, wanasema ni vigumu kufahamu ni nani ataibuka mshindi.
Wachambuzi wa siasa za Senegal, wanasema ni vigumu kufahamu ni nani ataibuka mshindi. © RFI/Melissa Chemam
Matangazo ya kibiashara

Wapiga kura wapatao Milioni 7.3 wakiwemo wale wanaoishi nje ya nchi, watashiriki kwenye zoezi hilo kumchagua kiongozi wao mpya, kumrithi rais Macky Sall, anayemaliza muda wake.

Ijumaa ndio ilikuwa siku ya mwisho ya kampeni ambapo wagombea 17, walizunguka maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi, kuwashawishi wapiga kura kuwapigia kura.

Wachambuzi wa siasa za Senegal, wanasema ni vigumu kufahamu ni nani ataibuka mshindi, na iwapo hilo litafanyika katika mzunguko wa kwanza, hata hivyo kufanyika kwa uchaguzi huo ni ahueni kwa raia wa nchi hiyo.

Hata hivyo, wagombea wawili wakuu ni Bassirou Diomaye Faye mwenye umri wa miaka 43, kutoka muungano wa kisiasa wa upinzani, anayeungwa mkono na mwanasiasa maarufu Ousmane Sonko, aliyezuiwa kuwania.

Mwingine ni Waziri Mkuu wa zamani Amadou Ba, mwenye umri wa miaka 62, anayeungwa mkono na rais anayeondoka madrakani Macky Sall.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.