Pata taarifa kuu

DRC: Mabasi ya Transco yasitisha shughuli zake kwa sababu ya ukosefu wa mafuta

Mji mkuu wa DRC, Kinshasa, unabeba mzigo mkubwa wa kutokuwepo kwa mabasi kutoka kwa kampuni ya usafiri wa umma (Transco). Kufuatia tatizo la ugavi wa mafuta wa serikali, kampuni inayosafirisha wakazi wa Kinshasa kwa bei nafuu inatatizika kwa shughuli ya usafirishaji wa watu. Suala hilo lilijadiliwa wikendi iliyopita wakati wa kikao cha baraza la mawaziri, lakini mgogoro huo bado haujatatuliwa.

Huko Kinshasa, basi ya kampuni ya Transco, kampuni ya serikali ya uchukuzi wa watu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Huko Kinshasa, basi ya kampuni ya Transco, kampuni ya serikali ya uchukuzi wa watu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Junior D. Kannah / AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa

Kampuni ya Transco ina mabasi 250 yanayotumwa kila siku kwenye barabara za Kinshasa, lakini kwa wiki kadhaa, ni dazeni chache tu ambazo zimeondoka kwenye eneo la maegesho. Baada ya serikali kuanza kutoa fedha wikendi hii, kampuni hiyo iliweza kuruhusu mabasi 110 pekee kati ya 250 kurudi barbarani na kuendelea na shughuli ya usafirishaji wa watu mjini Kinshasa, anaeleza mmoja wa maofisa wa kampuni hiyo.

Wateja walipata madhara siku ya Jumatatu. Msururu wa watoto wa shulewakiwa wanasubiri mabasi ya kampuni hiyo ilionekana kwenye barabara za mji mkuu asubuhi, huku watumishi wa umma wakijazana kwenye mabasi ya watu binafsi ambayo yanajulikana kama "safari ya kifo". Hali hiyo ni neema kwa waendesha pikipiki za kukodiwa ambazo zimenufaika kwa kuongeza maradufu bei ya nauli.

Kampuni ya Transco inakosa mafuta kwa mabasi yake, lakini matatizo ni magumu zaidi. Serikali inatarajiwa kulipa karibu dola milioni 1 kila mwezi kwa kampuni kama ruzuku ya mafuta na vipuri.

Fedha za kufidia hasara kampuni ya Transco inayopitia kwa kutoa huduma zake mara 4 hadi 6 kwa bei nafuu. Lakini kwa miezi kadhaa, Serikali haijalipa tena ruzuku zake. Kama vile marupuupu ya dola milioni 1.7 ambazo kampuni inapaswa kupokea kwa miaka miwili kwa usafirishaji wa abiria wasiolipa kama vile wanajeshi, polisi na wafanyakazi wa shirika la Msalaba Mwekundu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.