Pata taarifa kuu

Eritrea: Rais Afwerki amekutana na mgeni wake rais wa Somalia Sheikh Mohamud

Nairobi – Rais wa Eritrea Isaias Afwerki amefanya mazungumzo na mgeni wake rais wa Somali Hassan Sheikh Mohamud katika mji mkuu wa nchi hiyo Asmara.

Rais wa Somali Hassan Sheikh Mohamud anazuru nchi ya Eriteria
Rais wa Somali Hassan Sheikh Mohamud anazuru nchi ya Eriteria AP - Evelyn Hockstein
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya kigeni wa Eriteria Yemane Meskel, viongozi hao wawili walijadiliana kuhusu masuala ya ukanda likiwemo suala la Somalia kupambana na makundi ya watu wenye silaha.

Aidha shirika la habari linalomilikiwa na serikali ya Somalia limeeleza kuwa wakuu hao pia walijadiliana kuhusiana na masuala ya kimataifa bila ya kutoa taarifa zaidi.

Hii ilikuwa ziara ya pili ya rais Mohamud nchini Eritrea mwaka huu na ya sita tangu aiingie madarakani mwezi Mei mwaka wa 2022.

Hatua hii imetajwa kuwa ishara ya kuimarika kwa uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Rais Mohamud alizuru Asmara mwezi Januari wakati wa kipindi cha mzozo na jirani yake Ethiopia kuhusiana na makubaliano ya bandari kati ya Addis Ababa na Somaliland. Makubaliano ambayo hata hivyo yamepingwa na serikali ya Somalia.

Eritrea imekuwa ikitoa mafunzo kwa maelfu ya wanajeshi wa Somalia kama njia moja ya kuimarisha kikosi chake kuelekea kumalizika kwa muda wa ujumbe wa walinda amani wa AU katika Pembe ya Afrika mwishoni mwa mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.