Pata taarifa kuu

Somalia : Al Shabab wameshambulia hoteli maarufu karibu na makaazi ya rais

Nairobi – Magaidi wa Al Shabab wameshambulia hoteli maarufu karibu na makaazi ya rais jijini Mogadishu nchini Somalia.

Al Shabab ambayo inashirikiana na Al-Qaeda imekuwa ikitekeleza mashambulio kulenga hoteli.
Al Shabab ambayo inashirikiana na Al-Qaeda imekuwa ikitekeleza mashambulio kulenga hoteli. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa usalama na walioshuhudia tukio hilo la Alhamisi wamesema, limetokea usiku wa Alhamisi, wakati magaidi wa Al Shabab waliokuwa wamejihami kwa silaha walipovamia hotel kwenye hotel ya SYL na kuanza kufwatua risasi.

Ahmed Dahir afisa wa usalama mjini Mogadishu wamesema magaidi hao walibomoa ukuta na kuvamia hotel na mpaka sasa hakuna taarifa za uhakika iwapo kuna watu waliouwa au kujeruhiwa.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa wakati wa tukio hilo, kulikuwa na watu wengi kwenye hotel hiyo.

Al Shabab ambayo inashirikiana na Al-Qaeda imekuwa ikitekeleza mashambulio kulenga hoteli, viongozi wa juu wa Somalia na wale wa kigeni kwa kipindi cha miaka 16 sasa.

Shambulio hili linakuja siku moja baada ya Marekani kuwawekea vikwazo watu 16 na mashirika mbalimbali kwenye nchi za pembe ya Afrika na Mashariki ya Kati, kwa madai ya kuwaunga mkono Al Shabab.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.