Pata taarifa kuu

Senegal: Ousmane Sonko ameachiwa huru kutoka gerezani

Nairobi – Mpinzani nambari moja nchini Senegal, mwanzilishi wa chama kilichovunjwa cha Pastef, Ousmane Sonko, na luteni wake mwaminifu na mgombeaji wa uchaguzi wa urais wa Machi 24, Bassirou Diomaye Faye, wameachiliwa huru na kutoka katika gereza la Cap Manuel Alhamisi jioni ambapo maelefu ya watu walijitokeza kuwalaki.

Wafuasi wa Ousmane Sonko jijini Dakar.
Wafuasi wa Ousmane Sonko jijini Dakar. © JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko waliojitokeza kumlaki wakati akiondolewa gerezani kufuatia sheria ya msamaha iliopitishwa na bunge kwa makosa yaliofanywa wakati wa vurugu za maandamano.

Ousmane Sonko akiwa na mgombea mwenza Basirou Diomaye Faye waliachiliwa siku 10 kabla ya  uchaguzi wa rais. Waliondoka katika gereza la Cap Manuel kwa gari lililokuwa na vioo vya giza muda mfupi kabla ya saa sita usiku.

Mara tu alipoondoka gerezani, msafara wa makumi ya magari ulichukua barabara kuelekea Cité Keur Gorgui, wilaya ya Dakar ambako Ousmane Sonko anaishi, na hivyo kusababisha msongamano mkubwa wa magari na maandamano ya moja kwa moja.

Ousmane Sonko alikamatwa mwishoni mwa Julai baada ya shutuma za wito wa uasi, miongoni mwa mengine.
Ousmane Sonko alikamatwa mwishoni mwa Julai baada ya shutuma za wito wa uasi, miongoni mwa mengine. AFP - JOHN WESSELS

Njiani, mamia ya watu, mabango yenye kung'aa yaliyo na rangi za Pastef kwenye mikono yao na bendera ya Senegal mikononi mwao, waliingia barabarani na kushangilia, wakipiga honi zao au wakipiga kelele kwa furaha,ya kuachiwa kwa wapinzani hao.

Bassirou Diomaye Faye alikamatwa mwezi Aprili kwa kudharau mahakama baada ya kuchapisha kwenye Facebook.

Ousmane Sonko alikamatwa mwishoni mwa Julai baada ya shutuma za wito wa uasi, miongoni mwa mengine. Waliachiliwa jana Alhamisi jioni kufuatia kupitishwa kwa wabungewa Senegal kwa sheria ya msamaha juu ya uhalifu uliofanywa wakati wa maandamano ambayo yalifanyika kati ya Februari 2021 na 2024.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.