Pata taarifa kuu

Nigeria kufungua tena mipaka yake na nchi ya Niger

Nairobi – Rais Bola Tinubu amethibitisha kuwa Nigeria itafungua tena mipaka yake na Niger na kuondoa vikwazo vingine kwa jirani yake wa kaskazini, chini ya mwaka mmoja baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyotekelezwa na jeshi.

Mali, Niger na Burkina Faso walikuwa wametangaza mapema kujiondoa Ecowas baada ya vikwazo hivyo kuwekewa
Mali, Niger na Burkina Faso walikuwa wametangaza mapema kujiondoa Ecowas baada ya vikwazo hivyo kuwekewa REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Kilichozingatiwa hasa ni uamuzi wa jumuiya ya kikanda ya Ecowas kuondoa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya serikali ya kijeshi ya Niger, ambayo ilimpindua na kumweka kizuizini Rais Mohamed Bazoum mnamo Julai 6 2023.

Aliamuru kufunguliwa mara moja kwa mipaka, kuanza tena kwa safari za ndege za kibiashara na usambazaji wa umeme nchini Niger.

Mauzo ya nje yakiwemo mifugo na vitunguu kutoka Niger hadi Nigeria yamepungua kwa kiasi kikubwa.

Niger nayo pia imekumbwa na ukosefu wa bidhaa muhimu, huku jumuiya za mpakani zikiathirika zaidi na vikwazo hivi.

Mwezi uliopita, Ecowas, lilikubali kuondoa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Niger, Mali, Burkina Faso na Guinea ambazo zote zimeshuhudia mapinduzi ya kijeshi katika miaka miwili iliyopita.

Mali, Niger na Burkina Faso walikuwa wametangaza mapema kujiondoa Ecowas baada ya vikwazo hivyo kuwekewa.

Rais aliyepinduliwa wa Niger Mohamed Bazoum amezuiliwa na viongozi wa kijeshi nchini Niger tangu mapinduzi ya Julai mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.