Pata taarifa kuu

Senegal: Kampeni kuelekea uchaguzi mkuu zimeanza

Nairobi – Kampeni za uchaguzi wa urais nchini Senegal, kuelekea uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 24 mwezi Machi, zimeanza leo.

Rais Macky Sall, ambaye anamalizia muhula wake wa pili, anatarajiwa kuondoka madarakani ifikapo Aprili tarehe 2
Rais Macky Sall, ambaye anamalizia muhula wake wa pili, anatarajiwa kuondoka madarakani ifikapo Aprili tarehe 2 REUTERS - JOHANNA GERON
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inamaliza sintofahamu ya kisiasa iliyogubika taifa hilo la Afrika Magharibi, baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi uliokuwa ufanyike baadaye mwaka huu, lakini ukapata pingamizi kubwa kutoka ndani nan je ya nchi hiyo.

Kwa wiki kadhaa kulikuwa na maandamano makubwa jijini Dakar yaliyogeuka kuwa makabiliano makali kati ya polisi na waandamanaji na kusababisha maafa na majeraha.

Wagombea 19 wanajitosa kwenye uwanja wa kisiasa kuomba kura, katika taifa hilo lenye watu Milioni 18 kampeni ambazo zitafanyika katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wanaharakti wamekuwa wakisisitiza uchaguzi huo kufanyika kama ilivyopangwa
Wanaharakti wamekuwa wakisisitiza uchaguzi huo kufanyika kama ilivyopangwa REUTERS - ZOHRA BENSEMRA

Rais Macky Sall, ambaye anamalizia muhula wake wa pili, anatarajiwa kuondoka madarakani ifikapo Aprili tarehe 2, wakati unaominiwa kuwa, nchi hiyo itakuwa imempata kiongozi mpya.

Siku ya Ijumaa, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na Marekani, zilipongeza hatua ya kupangwa kwa tarehe mpya ya uchaguzi haraka, kitendo kilichosifiwa kama jitihada za Senegal kuendeleza rekodi yake ya kuwa mfano wa nchi zenye demokrasia thabiti barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.