Pata taarifa kuu

DRC: Mwendesha mashtaka apendekeza kifungo cha miaka 20 dhidi ya Stanis Bujakera

Nairobi – Nchini DRC, Mwendesha mashtaka wa kesi dhidi ya mwandishi wa habari Stanis Bujakera, amependekeza kifungo cha miaka 20 jela dhidi ya mwandishi huyo aliyekamatwa na polisi jijini Kinshasa Septemba 8 mwaka 2023.

Tangu kukamatwa kwa Stanis Bujakera, mashirika kadhaa ya kutetea haki za kibinadamu yamekuwa yakiomba kuachiwa huru kwa mwanahabari huyo
Tangu kukamatwa kwa Stanis Bujakera, mashirika kadhaa ya kutetea haki za kibinadamu yamekuwa yakiomba kuachiwa huru kwa mwanahabari huyo © Avec l'aimable autorisation de actualite.cd
Matangazo ya kibiashara

Miezi sita tangu kukamatwa kwake, mwendesha mashtaka Serge Bashonga, aliomba ahukumiwe kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kutoa taarifa za uongo na kueneza uvumi.

Mwandishi huyo wa habari wa Jeune Afrique, alikamatwa Septemba 8 akidaiwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu ripoti iliyochapiswa na Jeune Afrique ikihusisha ujasusi wa kijeshi katika mauaji ya aliyekuwa waziri wa zamani Chérubin Okende.

Mahakama itatoa uamuzi wake tarehe 20 ya mwezi huu, kwa mujibu wa mkuu wa mahakama. Tayari upande wa utetezi umepinga mashtaka yote dhidi ya Bujakera.

Tangu kukamatwa kwa Stanis Bujakera, mashirika kadhaa ya kutetea haki za kibinadamu yamekuwa yakiomba kuachiwa huru kwa mwanahabari huyo.

Tarehe 22 Februari, Rais wa DRC, Félix Tshisekedi, alisema atafuatilia kwa karibu suala hili la kuzuiliwa kwa mwandishi huyo wa habari.

Freddy Tendilonge/ Kinshasa/RFI Kiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.