Pata taarifa kuu

Nigeria: Wanafunzi zaidi ya 200 watekwa na watu wenye silaha

Nairobi – Watu wenye silaha wamewateka zaidi ya wanafunzi 200 kaskazini mwa nchi ya Nigeria kwenye mji wa Kuriga, mamlaka na mmiliki wa shule ambayo wanafunzi hao walichukuliwa, wamethibitisha.

Serikali ya Nigeria imekuwa ikipambana na watu wenye silaha wanaowateka watu na kuitisha kikombozi.
Serikali ya Nigeria imekuwa ikipambana na watu wenye silaha wanaowateka watu na kuitisha kikombozi. AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Hii ni idadi nyingine kubwa zaidi ya wanafunzi kutekwa tangu tukio la mwaka 2021 katika Shule ya Chibok, pia kaskazini mwa nchi hiyo.

Licha ya kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, Polisi kwenye jimbo la Kaduna, hawajatoa taarifa zaidi katika tukio lililotekelezwa maajira ya asubuhi wakati wanafunzi wakiwa wamemaliza mkutano wa asubuhi.

Hata hivyo kumekuwa na taarifa kinzani kuhusu idadi kamili ya wanafunzi waliochukuliwa mateka, baadhi wakisema 187 na wengine wakidai ni 40, wazazi wakilaumu tukio hilo kutokana na utovu wa usalama.

Tayari mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za bindamu, yamezitaka mamlaka za Nigeria kuhakikisha wanafunzi hao wanapatikana, ambapo huenda watekaji wakataka kulipwa kiasi cha fedha ili kuwaachia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.