Pata taarifa kuu

Mataifa mbioni kuweka pamoja rasimu ya mkataba mpya wa kimataifa wa majanga

Mataifa ya dunia yapo mbioni kupata mwafaka kuhusu maguezi yanayopendekeza kwenye mkataba mpya wa kimataifa kuhusu namna ya kupambana na majanga ,utakaopitishwa kwenye kongamano la kimataifa Geneva mwezi Mei.

Makao makuu ya shirika la afya duniani
Makao makuu ya shirika la afya duniani © Reuters - Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara
01:51

RIPOTI YA RASIMU YA MKATABA WA MAJANGA

Baada ya janga la Uviko 19 lilosibu mataifa yote ya ulimwengu,shirika la afya duniani lilipendekeza kufanyika marekebisho kwenye sheria ya kukabiliana na majanga kwa njia ya nchi kuja na mkataba  mmoja kuhusu majanga kabla kongamano la afya duniana mwezi Mei

Shirika la afya duniani limekuwa likihimiza mataifa wanachama kutoacha nyuma kwenye mchakato huo ulionza mwaka  2021 baada ya kongamano la afya duniani ,kuunda taasisi inayoleta pamoja serikali mbali mbali za dunia kuendesha mazungumzo na kuja na mwafaka kuboresha mikakati ya kupambana na majanga

“ Tupo kwenye mchakato wa mwisho wa rasimu ,ni muhimu mataifa wanachama kushiriki,wajua kwenye mikutano ya kifamilia,ni hatari kusema hutoshiriki,wataamua kwa niaba yako na mara nyingi si kukupendelea,”alisihi Martins Livinus mratibu wa huduma za dharura WHO nchini Kenya.

Nchi mbali mbali zimekuwa zikilamamikia kulemewa na COVID 19 kwa kuwa mifumo ya afya haikuwa thabiti.

Dkt Martin Sirengo anaratibu uhusiano kati ya wizara ya afya Kenya na mashirika ya kimataifa

“ Hii ni kutokana na mafundisho ambayo tulipata wakati wa Covid 19,ingawaje kulikuwa na mipangilio  imewekwa na WHO ya kukabiliana na majanga kimataifa ,kulikuwa na changamoto hapa na pale,WHO ikaweka kamati inayohusisha watalaam kutoka nchi mbali mbali wa kupambana na majanga,”alielezea Daktari Martin Sirengo.

 

 Baadhi ya mapendekezo kwenye  rasimu ya mkataba huo , ni swala la usawa ,ufadhili ,será moja ya afya  duniani na hakimiliki .

Mataifa ya Afrika yanahoji  kutokana na uwezo tofauti wa kimapato ,nchi za magharibi zinapaswa kuwaruhusu kuchangia kulingana na uwezo wa kifedha.

Na kwenye michango yao katika ufumbuzi wa dawa au chanjo mpya ,kuwe na mwongozo kuhusu faida kutokana na juhudi zao .

Kibet Kisorio ni mwanasheria katika bodi ya udhibiti  dawa katika wizara ya afya.

“Tulishuhudia changamoto nyingi kupata dawa wakati wa Covid 19 ,barakoa na mambo mengi, sasa kwa haya majadiliano tunatafuta mkataba ambao utaamua  au kupeana maelekezo janga likitokea,”alisema Kibet Kisorio

Mashirika ya kiraia pia yanashinikiza biashara ya chanjo mpya na haki za binadaam kuwekwa bayana.

Aggrey Aluso anawakilisha muungano wa mashirika ya kiraia kuhusu majanga ukanda wa Afrika.

“Ili tuwe na njia nzuri ambayo italeta usawa katika uwezo wa kukabiliana na majanga,lazima nchi zishirikiana na lazima tusiweka mbele biashara ,tuweke haki ya kibinadaam mbele,”alisihi Aggey Aluso.

Shirika la afya limekuwa likizionya nchi mbali mbali kujiandaa kwa majanga wakati wowote baada ya Corona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.